Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar
Mwakilishi
Mkaazi wa Shirika la Kimataifa linaloshuhulikia Idadi ya watu Duniani
UNFPA Jaqline Mohan amesema Shirika lake litaendelea kutoa mashirikiano
katika sekta ya afya hasa katika uzazi salama ili kuweza kuyanusuru
maisha ya mama na mtoto.
Hayo
ameyasema huko katika ofisi ya Wizara ya Afya Mnazi Mmoja wakati
alipokuwa akielezea lengo la matarajio yao katika kusaidia mpango wa
uzazi salama wa mama na mtoto.
Alisema
afya na mama na mtoto ni muhimu katika jamii hivyo wataendelea kusaidia
sekta hiyo ya afya ili kuhakikisha kuwa kinamama wanapata huduma bora
wakati wa kujifungua pamoja na watoto kupata makuzi yaliyo salama ili
kupunguza vifo wakati wa uzazi.
Alisema
vifo vingi vya akinamama na watoto hutokea wakati wa kujifungua hivyo
huduma hiyo itaweza kupunguza vifo na kusaidia kuwapa uzazi salama kwa
kujenga afya bora na makuzi mazuri wa watoto.
“Tuna
mpango wa kusaidia Wizara ya Afya katika mambo ya kijamii , uzazi
salama kwa mama na mtoto na kushuhulikia vijana katika kujua afya zao”
alisema mwakilishi huyo.
Alieleza
kuwa Shirika lake pia lina lengo la kuwasaidia vijana kwa kuhakikisha
kuwa wanaishi na afya bora , kuwapa uhuru wa kujipanga katika kujiletea
maendeleo yao pamoja na kuwasaidia kwenye mambo ya kiuchumi. kwani ndio
nguvu kazi ya Taifa
Nae
Waziri wa Afya Hamadi Rashid Mohammed amelishukuru shirika hilo kwa
kutoa mashirikiano katika kuboresha afya za mama na watoto katika uzazi
ulio salama.
Alisema
watazidi kushirikiana kwenye kutoa elimu zaidi ya uzazi wa mpango ulio
salama ili kupunguza vifo vya mama na mtoto, kwani elimu ya uzazi bado
uzazi wa mpango iko chini na kuwataka akinamama kuwa na muamko wa
kupanga uzazi ilikunusuru maisha yao pamoja na kuwa na afya bora
“Elimu
inahitajika zaidi kwa jamii na iendelee kutolewa katika suala zima la
uzazi wa mpango salama kwa mama na mtoto na pia kuwashauri akina baba
kuwapa fursa akina mama kujiunga na uzazi salama”, alieleza Waziri Hamad
.
Waziri
Hamad alisema shirika hilo limesaidia kutoa dawa kwa ajili ya jamii
ikiwemo vifaa vya uzazi kwenye wodi ya uzazi katika Hospitali ya Mnazo
Mmoja na mwembeladu pamoja na kutoa mafunzo wafanyakazi ili waweze
kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“
Uzazi wa mpango ulio salama umo mpaka katika vitabu vya dini yetu ya
kiislamu hivyo tujitahidini ili kuweza kuleta afya iliyo bora kwa mama
na mtoto na kupata nguvu ya kulea mtoto miaka miwili na kupumzika
angalau mwaka mmoja”, alisema Waziri huyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Ali Salim alisifu jitihada
wanazozitoa shirika hilo katika kuboresha sekta ya afya ya mama na mtoto
jinsi wanavyoweza kutoa juhudi za Afya za mama na mtoto katika kuweka
uzazi ulio salama.
MWAKILISHI
wa UNFPA Tanzania Jacguline Mahon akizungumza na Waziri wa Afya
Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kuhusu kuongeza ushirikiano juu ya uzazi
salama na kuimarisha afya ya Mama na Mtoto, (kulia kwake) ni Mwakilishi wa (UNICEF) Maniza Zaman
WAZIRI
wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wawakilishi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja
Mjini Zanzibar.
WAZIRI
wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed katika akipiga picha ya pamoja na
Wawakilisi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, (kushoto) Mania
Zaman wa UNICEF na Jacguline Mahon wa UNFPA (Picha na Abdalla Omar Maelezo - Zanzibar).
No comments:
Post a Comment