NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama aliyevaa koti jeupe
Nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi akiwa amelishikilia kombe lao kulia ni NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akimvalisha medali mchezaji wa timu ya Ushirika FC ambao walishika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kombe la Aweso Cup kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akimkabidhi sh.50000 Twaha Bungala ambaye ni mfungaji bora kwenye mashindano hayo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso katikati akimkabidhi kitita cha sh.milioni 1 nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi juzi ambao niMabingwa wa Ligi ya wilaya hiyo maarufu kama Aweso Cup iliyodhaminiwa na Mbunge huyo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)akizungumza wakati akifunga mashindano hayo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati akifurahia jambo na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa mechi ya fainali
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakifuatilia mechi ya Fainali ya Ligi ya Aweso Cup kulia ni Abdul Ubinde kutoka Klabu ya Coastal Union
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Pangani (PDFA) wakifuatilia mchezo wa fainali ya Ligi ya Aweso Cup
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM akikagua timu shiriki kabla ya kuanza mchezo huo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na timu shiriki kabla ya kuanza mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Kumba wilayani Pangani
Viongozi wa timu ya Coastal Union "Wagosi wa Kaya"wakifuatilia mechi hiyo ya fainali kulia ni Salim Bawaziri ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na kushoto ni Abdul Ubinde
KIKOSI cha timu ya Ushirika FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi hiyo.
TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani Pangani.
TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).
Huku mshindi wa pili timu ya Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.
Aidha zawadi nyengine zilitolewa ni timu yenye nidhamu ambapo Super Boys ya Sakura ilifanikiwa kuibuka na kukabidhiwa seti jezi moja huku nafasi ya mfungaji bora ikichukuliwea na Twaha Bungala ambaye alikabidhiwa kitita cha sh.50, 000 wakati mwamuzi bora akiibuka Bakari
Juma “Enye” ambaye alipata Jezi ya waamuzi seti moja.
Ligi hiyo ilishirikisha timu 20 ambazo zilichuana vilivyo ili kuwezakumpata bingwa ambaye atapata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mkoa wa Tanga inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Akizungumza mara kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema ataendelea kusapoti michezo kwenye Jimbo lake ili kuweza kuwasaidia vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao sambamba na kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia soka ili waweze kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.
"Ndugu zangu wana Pangani hususani vijana michezo ni ajira hivyo tucheze mpira kwa malengo ikiwemo kujituma kwani hakuna mafanikio yanayoweza kuja bila kucheza kwa kuonyesha uwezo wenu kwa lengo la kufika mbali kisoka"Alisema.
No comments:
Post a Comment