Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amemuagiza mkuu wa Kituo Cha Polisi Gairo kuwakamata wale wote waliokula fedha za ujenzi wa maabara ya shule sekondari ya Idibo iliyiyopo katika Kata ya Idibo wilayani Gairo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara hizi karibuni Dkt. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona shilingi Milioni 12 fedha za ujenzi wa maabara zilizotokana na nguvu ya wananchi zinaliwa na watu wachache tena bila kufanikisha malengo.
"Hivi kuna watu bado hawaelewi umuhimu wa kutunza fedha za umma??? Haiwezekani wananchi wajichange harafu nyie viongozi wa kijiji mle hela zao za maendeleo bila aibu, siwezi kuvumilia... Nakuagiza OCD Gairo na TAKUKURU kufanya msako watu hawa wapelekwe mbele ya sheria haijalishi walishastaafu au la!," amesema. Amesema kuwa ni vyema kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuchangia maendeleo ya kijiji chao ila wanapotokea viongozi ambao si waaminifu ni vyema kuwaondoa haraka.
"Haiwezekani tokea mwaka 2014 maabara haijakamilika imeishia kujengwa msingi na kupandisha matofali kidogo huku fedha na nguvu za kujitolea wanachi ziwe zimepotea bure, naagiza viongozi waliokuwepo kipindi hicho wajisalimishe wenyewe huu ujinga hauwezi kuvumilika," amesema. Aidha mbali na madudu hayo aliyoyakuta Dkt. Kebwe alitoa pongezi zake za pekee kwa uongozi wa wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe kwa kuweza kusimamia vyema maendeleo ya wilaya na kuona inavyokuwa kwa haraka.
Amesema wilaya ya Gairo ilianzishwa mwaka 2013 lakini imeonyesha kuwa na miradi mingi ya maendeleo ambayo iko hai jambo linalompa faraja sana kwa kuona viongozi wanachapa kazi. "Wanawake wanaweza kweli, wilaya yenu inaongozwa na akina mama na wanachapa kazi vizuri sana, kwa hili lazima niliseme bila hata kificho... mpe mtu sifa zake akiwa hai maana hawa ndiyo wasaidizi wangu najua wanapitia changamoto nyingi ila wanazipangua na kusonga mbele,' amesema. Akihitimisha Dkt. Kebwe amewaasa wananchi kujitunza ili kuweza kuepuka magonjwa nikiwemo gonjwa la UKIMWI, mimba kwa watoto wa shule.
"Nimeambiwa na Madiwani wenu kata yenu inaongoza kwa maambukizi ya VVU na kuwapa mimba watoto wa shule jambo ambalo ni hatari, tunakwenda kupoteza nguvu kazi tusipokemea haya mtazidi kuuana kila kukicha, acheni ngono zembe tumieni kinga ili mnusuru na vizazi vyenu," amesema. Awali akitoa mrejesho Diwani wa Kata Idibo ametoa shukrani kwa uongozi na kuomba wazidi kuwaomba wananchi wajitolee zaidi ili kutimiza malengo yao ya ujenzi wa sekondari, kituo cha polisi.
"Mheshimiwa kuna vijiji vimegoma kuchangia maendeleo ya kata yetu jambo linalodhoofesha ukuaji wa kata yetu, nikuombe utie msisitizo ili mambo yaende salama," amesema. Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amemaliza ziara yake ya kukagua maendeleo katika Wilaya ya Gairo ambapo alianzia katika Kijiji cha Tabu Hoteli, na kukagua mradi wa maji wa Ihenje baadae alikwenda Iyogwe na Itarage ambapo alikagua ujenzi wa kisima cha maji.
Vile vile Alikagua kituo cha afya cha Gairo. Baadae Dkt. Kebwe ameweka jiwe la msingi majengo ya shule ya msingi Chagongwe na kukagua daraja ndipo alipoelekea kukagua shule ya Nongwe na kujionea eneo itakapojengwa Kidato cha tano na sita. Siku ya mwisho ali alifanya usafi soko la Chakwale, akahamasisha ujenzi wa sekondari ya Chakwale na kumalizia katika kijiji cha Idibo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwahutubia wakati kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (wa tano toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (kulia kwake), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kulia kwa mkuu wa mkoa) pamoja na wengine. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea zawadi ya mahindi mara baada ya kuwahutubia (katikati) wananchi wa kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akisikiliza maelezo mafupi ya ujenzi wa shule ya Idibo ulioanza mwaka 2014 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekwama katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiongozwa na Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Idibo unaoendelea mpaka sasa katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi pamoja na pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya kijiji wakiwa katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), wakiwa katika shamba la shule ya sekondari Idibo kujionea jinsi ulimaji wa zao la pamba ulivyopamba moto katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akikagua ujenzi wa kituo cha polisi katika Kata ya Idibo ulioanza mwaka 2014 na mpaka leo unasua sua jambo lililomsikitisha Mkuu wa Mkoa na kuagiza wale wote wanaohusika wamalizie haraka iwezekanavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kushoto) pamoja na OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Kipingu wakikatisha katika mitaa ya kijiji cha Chakwale kuelekea Soko la Chakwale kwa ajili ya usafi katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakifanya usafi katika Soko la Chakwale kwa ajili ya usafi katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Kipingu nae hakuwa nyuma kufanya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (katikati) pamoja na mwenyekiti wa wazazi CCM (aliyeshika tolori) wakikusanya uchafu katika Soko la Chakwale iliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Adam Bibangamba (aliyeshika tolori) akipita kukusanya uchafu.
(aliyeshika tolori) akikusanya takataka.
Zoezi la kukusanya takataka likiendelea.
Viongozi walioambatana na Mkuu wa Mkoa nao hawakuwa nyuma kufanya usafi. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiongea na wananchi wa Kijiji cha Chakwale juu ya ujenzi wao wa shule ya sekondari. Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Adam Bibangamba akizungumza salamu za utangulizi wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Chakwale, Wilayani Gairo. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akicheza muziki na viongozi wa wilaya ya Gairo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto). Meza kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Chakwale wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe alipofanya ziara yake Wilayani Gairo kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (aliyeshika tolori) akikusanya takataka. Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno akitoa kero zinazowakumba wananchi wa Chakwale. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
No comments:
Post a Comment