Friday, June 1, 2018

Prof.Mkenda afanya ziara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Namanga


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na wajumbe (hawapo pichani)  waliohudhuria kikao baina yake, watendaji wa Kituo hicho na wafanyabiasha wanaozunguka eneo hilo kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo.Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya.
Wawili hao kwa pamoja sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu katika kituo hicho.
Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo
 kurahisisha shughuli za biashara.
 Vilevile ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi wanaotumia kituo hicho.
Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza M
amlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi. 

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya (kushoto), kenye kikao cha wadau kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa OSBP ya Namanga 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (watatu kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa nana Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila (kushoto) na Mwenyeketi wa Wafanyabiasha Namanga  (katikati) wakiwa katika ziara za kutembelea kituo cha  OSBD 

Mhe.Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya akizungumza katika Kikao

Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila akizugumza wakati wa kikao

Mmoja wa Maafisa wanaohudumu katika OSBP ya Namanga akitoa mada kwa makatibu wakuu na wajumbe wengine wa mkutano juu ya utendaji wa kituo hicho

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  akizungumza na wajumbe wakati wa kikao

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Namanga akizungumza wakati wa kikao

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya katika ziara ya kutemebelea OSBP Namanga
Bw.Edwin Iwato Meneja Msaidizi Mkoa,Forodha Arusha akitoa neno la kuwakaribisha Makatibu Wakuu na Wajumbe wengine waliofika kwenye ziara katika Kituo cha OSBP Namanga

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliombatana nao kwenye ziara 



No comments: