Wednesday, June 6, 2018

NAIBU WAZIRI WA ARDHI ANGELINA MABULA AANZA ZIARA MKOA WA LINDI NA KUHIMIZA ULIPAJI KODI YA ARDHI ASULUHISHA MGOGORO BAINA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA KICHONDA LIWALE MKOA WA LINDI NA MUWEKEZAJI

Na Munir Shemweta, Liwale
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesuluhisha mgogoro ulipo katika kijiji cha Kichonda kilichopo wilayani Liwale mkoa wa Lindi baina na wakazi wa kijiji hicho kuhusu uhawishaji wa ardhi ya kijiji ekari 1000 kwenda kwa muwekezaji M/S KSM & AGL EXPORT FARM C LTD.Wananchi wa kij
iji cha Kichonda wamekataa uhawishaji wa ardhi ya kijiji hicho kwenda kwa muwekezaji kwa madai kuwa muwekezaji huyo ameshindwa kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa kwa wakazi hao kabla ya kumilikishwa rasmi eneo hilo.
Kwa mujibu wa wakazi wa kijiji hicho, muwekezaji huyo aliwaahidi wakazi hao kuwajengea msikiti, kuwachimbia kisima cha maji, kusaidia magodoro katika zahanati ya kijiji lakini wamedai kuwa kutotekelezwa kwa ahadi zote hizo kumewafanya kukosa imani naye na kueleza kuwa hastahili kumulikishwa eneo hilo.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walieza kuwa, muwekezaji huyo kwa sasa hapaswi kulaumiwa kwa kuwa eneo lenyewe hajapewa jambo linalomuwia   vigumu kwake kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa hivyo walitaka akubaliwe kumilikishwa ndipo waanze kumlaumu.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Omar Saidi alisema muwekezaji huyo anawashangaza sana kwani ameahidi kufanya mambo mengi lakini mpaka leo anaonekana kimya hivyo kwao wanaona kama anawababaisha.
Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula ametembelea kijiji hicho cha Kichonda kwa lengo la kuhakiki uhawishaji wa eneo hilo kabla ya maombi kuwasilishwa kwa mhe rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili aweze kuridhia.
Akizungumza na wanakijiji wa Kichonda katika mkutano wa hadhara Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwaeleza kuwa, uamuzi wa wao kuridhia uhawishaji shamba hilo hakumpi fursa ya moja kwa moja muombaji kuwa mmiliki bali kuna hatua mbalimbali za kupitia kisheria kabla ya kumilikishwa.
Mhe Mabula aliyeambatana na Kamishna Msaidizi wa ardhi kanda ya kusini Gasper Luanda, Kaimu Kmaishna wa ardhi vijijini Kokwika Ishenkumba na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Liwale na mkoa wa Lindi aliwaambia wakazi wa kijiji hicho kuwa uhaulishaji ni ‘’process’’ ndefu na kwamba hata mhe rais akikubali lazima mchakato upitie taratibu zote za kisheria ikiwemo kutolewa siku tisini kwa muwekezaji kukaa na wana kijiji ili kukubalina.
Kufuatia maelezo hayo ya mhe mabula, wananchi wa kijiji cha Kichonda walibadili maamuzi yao ya kukataa eneo hilo kuhaulishwa kwa mwekezaji huyo aliyeomba ambaye awali wana kijiji walikubaliana apatiwe umiliki kwa ajili ya uwekezaji.

Ombi la Muwekezaji M/S KSM & AGL EXPORT kutaka kumilikishwa eneo la kijiji cha Kichonda ekari 1000 kwa ajili ya kuzalisha alizeti, kufuga nyuki, kuku, ng’ombe, mbuzi na samaki liliwasilishwa 2010 na uwekezaji huo umeelezwa kuwa utaisadia serikali kupata kodi sambamba na kupatikana huduma nyingine za kijamii pamoja na fursa ya ajira kwa wananchi wa eneo la kijiji.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia ofisi ya Baraza la Ardhi mkoani Lindi wakati wa ziara yake ya siku mbili kukuagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi jana.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiangalia Majalada wakati alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoa wa Lindi jana.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Andrew Munisi (Kushoto) kuhusiana na makusanyo ya kodi ya ardhi, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Denis Masame
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa halamshauri ya Manispaa ya Lindi, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemaga na kushoto ni mbunge wa Viti Maalum Hamida Abdallah (Picha na Munir Shemweta- WANMM).
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kichonda wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi  wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji hicho kwa muwekezaji.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kichonda wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (hayupo pichani) wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kichonda wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (hayupo pichani) wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji.
 Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper Luanda akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kijiji cha Kichonda wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi.
 Kaimu Kamishna wa Ardhi vijijini Kokwika Ishenkumba akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kijiji cha Kishonda wakati wa zoezi la uhakiki wa uhaishwaji eneo la ekari 1000 uliofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi.
 Diwani wa Kichonda wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi akitoa maoni yake wakati wa kikao baina ya wananchi wa Kichonda na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Angelina Mabula.
 Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kichonda akichangia maoni wakati naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi alipotembelea kijiji hicho kuhakiki zoezi la uhaishwaji ekari 1000 kwa muwekezaji.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akisalimiana na akina mama mara baada ya kuwasili wilaya ya Liwale mkoa Lindi kwa ajili ya kutembelea kijiji cha Kichonda. (Picha zote na Munir Shemweta- WANMM)

No comments: