Monday, June 25, 2018

Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa wafanyika jijini Arusha

Mkutano huu unaofanyika kila mwaka, mwaka huu pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa za utelelezaji wa mapendekezo, maagizo na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na kuamuliwa katika mikutano ya ngazi mbalimbali na vyombo vya kisera vya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
 Sekta zinazotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na sekta ya miundombinu ya uchukuzi inayojumuisha aridhi, anga na maji, mawasiliano na hali ya hewa. 
 Utelezaji wa maagizo, mapendekezo na maamuzi mbalimbali yaliyotolewa ili kuboresha maeno haya unatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii katika nchi wanachama za Jumuiya Afrika Mashariki. 
 Mkutano huu unaoendelea jijini Arusha na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika katika ngazi tatu ambazo ni; ngazi ya Wataalam, ngazi ya Makatibu Wakuu na hatimaye ngazi ya Mawaziri.
Mhandisi Abdillah Mataka Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akichangia jambo kwenye mkutano wa  15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa unaondelea jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukiimbwa na wajumbe kabla ya kuanza kwa mkutano.
Sehemu ya wajumbe kutoka Tanzania wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa mkutano. Kushoto ni Mhandisi Abdillah Mataka Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii, Mhandisi Julius Chambo (katika) Mkurugenzi Sekta ya Ujenzi kutoka  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bw. Moses Malipula kutoka Wizara ya Fedha na Mipango

Meza kuu ikiongoza majadiliano wakati wa mkutano

Sehemu ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa.

Bibi Edna Chuku (wa kwanza kulia) Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea.

No comments: