Tuesday, June 5, 2018

MISS UBUNGO MWAKA 2014 DIANA KATO ASHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA AMANA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
ALIYEKUWA Miss Ubungo jijini Dar es Salaam mwaka 2014-2016 Diana Joachim Kato ameshiriki kuadhimisha wiki ya mazingira kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini.

Miss huyo ambaye ana mradi wake wa maji safi na salama amefanya usafi huo kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Ilala jijini Saady Khimji.Hivyo ameamua kushiriki siku ya mazingira duniani kwa kuamua kuitumia siku ya leo kufanya usafi hospitalini hapo ikiwa pamoja na kupanda miti.

Akizungumza baada ya kufanya usafi huo Diana Kato amesema ameamua kushiriki siku ya mazingira duniani kwa kufanya usafi katika hospitali hiyo pamoja na kupanda miti huku akiweke akitoa mwito kwa Watanzania kuendelea kutunza mazingira.

"Nimeona ni vema leo nikawa katika hospitali ya Rufaa ya Amana kwa ajili ya kufanya usafiti na baada ya hapo nikashiriki kupanda miti .Hii yote ni katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani .Kubwa zaidi nitoe rai kwa Watanzania tuwe sehemu ya kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha tunatunza mazingira yetu ili nayo yatutunze.
Aliyekuwa Miss Ubungo 2014/16,  Diana Joachim Kato akipanda mti katika  Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa  maadimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo
Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji  akipanda mti katika  Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo.
Baadhi ya vijana wakifanya usafi wamazingira yanayoizunguka Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo.
Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji(wa pili kushoto) na Aliyekuwa Miss Ubungo 2014/16,  Diana Joachim Kato(kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja walipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana  kwa ajili ya kupanda miti pamoja na kufanya usafi wa mazingira yanaoizunguka hospitali hiyo leo.

No comments: