Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akionyeshwa na Mkuu wa Gereza Chato, Joseph Busumabu, maeneo mbalimbali ya Gereza hilo ambalo tayari linahifadhi wafungwa na mahabusu na pia linaendelea kupanuliwa kwa kujengwa majengo mapya zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Shabaan Ntarambe. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulamboakimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Kituo kipya cha Polisi mjini Chato ambacho kipo katika hatua ya mwisho kukamilika. . Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoka kukagua ujenzi wa Gereza Chato, mkoani Geita, ambalo licha ya kua tayari Gereza hilo jipya limenza kuhifadhi wafungwa na mahabusu lakini linaendelea kupanuliwa kwa kuongezwa majengo zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, na kulia alyevaa sare, ni Mkuu wa Gereza hilo, Joseph Busumabu. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, mara baada ya kumaliza kukikagua Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Chato (nyuma pichani) ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya mwisho kukamilika. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi hicho, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) eneo la pembezoni mwa Ziwa Victoria ambalo linaweza kufaa kujengwa Kituo cha Polisi cha Wanamaji katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha ulinzi zaidi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Geita, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi zinazojengwa nje kidogo mwa mji wa Geita. Masauni alisema ujenzi wa nyumba hizo utapunguza ukosefu wa nyumba kwa askari wa mkoa huo mpya, hata hivyo nyumba zaidi ya elfu moja zinatarajiwa kujengwa mkoani humo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo. Masauni alifanya ziara mkoani humo kwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba hizo 100 kwa ajili ya makazi ya askari polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi, akimpa maneno ya kumuagaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo naye ofisini kwake, jana. Mkuu wa Mkoa huyo alimuambia Masauni wanashirikiana vizuri na vyombo vilivyopo ndani ya Wizara yake na hali ya ulinzi na usalama ipo vizuri mkoani humo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Selestine Gesimba. Masauni amemaliza ziara yake mkoani humo, ambapo alifanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment