Friday, June 8, 2018

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA ATEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA KIGAMBONI,AISIFU MAHAKAMA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MOLADI KTK UJENZI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro ameipongeza mahakama ya Tanzania kwa utekelezaji wa miradi ya mahakama kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya ujenzi wa bei nafuu ya mradi wa Molandi.

Pia Okoro ameipongeza mahakama kwa kuzingatia uwiano wa jinsia mahakamani katika utekelezaji wa majukumu kwani ameona kutoka ngazi za juu hadi ya chini wanawake wako wengi, 

Okiro amesema hayo leo Juni 8,2018 wakati anatembelea Mahakama ya Mwanzo na ile ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo alishuhudia majengo na kupewa maelezo mbali mbali yanayofanywa na mahakama za Tanzania. Ikiwemo mahakama inayotembea (Mobile Court).

Amesema taarifa za ujenzi wa majengo hayo ni za mfano wa kuigwa na zinapaswa kuwa mfano wa nchi nyingi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwani majengo hayo ni mazuri na yanakidhi thamani ya fedha.Amesema, taarifa ya namna ya mfumo wa mawasilisho na ujenzi na jinsi miradi hiyo inavyofanya kazi,ni mfumo mzuri na ni kitu cha kuigwa kwani inaonyesha wazi ni jinsi gani jengo lilivyo na mfumo mzuri.

"Nimefurahi sana, miradi imejengwa kwa mfumo mzuri, majengo nilikuwa nikiyaona kwenye documents tu lakini sasa hivi nimeyaona, yanakidhi vigezo na thamani ya pesa", amesema Okiro.

Kabla ya kuongea hayo, makamu wa rais huyo, alipata nafasi ya kusikikiza taarifa (Presentation) kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo (Court Mapping) kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula amesema, katika mahakama hiyo, wameweka mifumo ya mawasiliano ya kutoa taarifa mbali mbali za mahakama itakayomuwezesha mwananchi kufuatilia kesi bila ya kufika mahakamani, na vile vile ramani ya kufika mahakamani hapo kutokea mahali popote.

Kwa upande wake, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Joachim Tiganga, amesema, mahakama hiyo ya Kigamboni imekuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo kwani kwa sasa imewarahisishia upatikanaji wa haki kwani mwanzoni walikuwa wakisafirisha umbali wa kilomita 50 kwenda Temeke kufuata huduma ya Mahakama ya Wilaya.

Nae, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, alieleza jinsi teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kusema wamefanikisha ujenzi wa mahakama zaidi ya tano kwa Ambazo zilijengwa kwa muda mfupi na garama nafuu

Alizitaja mahakama hizo kuwa ni mahakama yav Bagamoyo na nyumba za watumishi, Kituo cha Mafunzo kilichoko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mahakama ya Kibaha, Kigamboni, Kawe na Mkuranga.
Amesema kupitia teknolojia hiyo bado majengo 16 yanaenselwa kujengwa katika mikoa mbali mbali hapa nchini.


Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo: Court Mapping kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula, akieleza jinsi mfumo wa kutoa taarifa mbali mbali za mahakama una vyofanya kazi katika Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni kupitia mradi wa Court Mapping. 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, akieleza jinsi teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kufanikisha kwa mafaniko makubwa mahakama zaidi ya tano zilizojengwa kwa muda mfupi na garama nafuu.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro (katikati) aliyevaa miwani akiwa katika Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro kulia akizungumza na wadau mbali mbali wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi. Pembeni yake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.

No comments: