KIJANA
wa miaka 18 kutoka Saudi Arabia, Ibn Rayizah Hatim Abdullah ameibuka na
kitita cha dola za Marekani 5,000 kwenye fainali za 26 za tuzo ya
Kimataifa ya Quran tukufu.
Kijana
Rayizah ameibuka na kitita hicho baada ya kuwashinda wenzake sita
waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Yemen, Zanzibar,
Malaysia, Mali, Marekani na Tanzania Bara.
Nafasi
ya pili imechukuliwa na kijana Hamza Soukouna (25) kutoka Mali ambaye
amejishindia dola za Marekani 4,000 na ya tatu imechukuliwa na Hamza
El-Habashiy (18) kutoka Marekani ambaye amejishindia dola za Marekani
3,000. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran
Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 16 kutoka nchi 16 duniani.
Akizungumza
na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee leo mchana (Jumapili, Juni 3, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amewataka viongozi wa dini hiyo waendelee kuwakamata vema vijana
waliohifadhi Quran na kuwaendeleza kitaaluma katika fani nyingine za
elimu ya kimazingira.
“Leo
hii nimefarijika sana kusikia kwamba tunao vijana wetu ambao si tu
wamehifadhi Quran bali pia wamehitimu fani mbalimbali katika elimu ya
juu. Uwepo wa vijana wa namna hii ni muhimu katika kujenga jamii bora na
yenye kuzingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao,” amesema.
Amesema
kazi ya kuhifadhisha Quran haiishii katika kujua kuisoma pekee.
“Kuhifadhisha Quran kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii
bora kupitia mafunzo sahihi ya tabia njema, utii lakini pia kujua mipaka
katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana
hawa tunaowahifadhisha Quran kuwa raia wema, wazalendo, wanaotambua wajibu wao, majukumu yao, kwao wenyewe na kwa nchi yao pia,” amesema.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wanaoendesha taasisi za
kuhifadhi Quran wakae pamoja na watengeneze ratiba ya mashindano ya
kitaifa na kimataifa ili waweze kuwa na mashindano yanayoanzia ngazi za
chini hadi za juu.
“Kaeni
pamoja, mtenge ratiba ya kuanzia ngazi ya kimataifa hadi kimataifa,
ratiba hizi zipangwe na kutambulika kitaifa. Wekeni ratiba ili washiriki
washindane kuanzia mikoani, ushindani uwepo na tuwaone wakipanda kutoka
mkoa, Taifa, Afrika Mashariki, Afrika hadi ya Dunia,” amesema.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Mufti wa
Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali alisema wameanza kuona matunda
ya kazi ya kuhifadhisha Quran kwani vijana wa Kitanzania wamesoma elimu
ya mazingira (circular education) na elimu ya dini na wamefaulu vizuri
sana.
“Sasa
hivi tunataka watoto wetu wafikie elimu ya juu ya dini na hii ya
mazingira. Tunawapongeza hawa vijana wa Kitanzania ambao walienda hadi
nje ya nchi kutafuta elimu ya juu na sasa wamerudi nyumbani kuasaidia
ndugu zao,” alisema.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, Sheikh Othman Ali
Kaporo alisema jumuiya ilianza kazi zake kimyakimya mwaka 1984 lakini
ilianza kujulikana mwaka 1992
Alisema
walianzisha jumuiya kwa sababu walibaini kuwa jamii ina kiu ya kupata
watu wema watakaochangia maendeleo wa Taifa. “Ukiangalia mwelekeo wa
vijana wetu wa Kiislamu si mzuri. Hebu fanya utafiti wa kina wa wale
waliokuwemo magerezani. Je tunaumizwa na jambo hili? Na kama tunaumizwa
tunafanya nini ili kuwaokoa vijana hawa? Haya ndiyo tunayalenga sisi, na
kwa kupitia Quran, tuweze kuwaokoa na majanga yale,” alisema.
“Kuna
vijana wengi wana vipaji lakini vinakufa kwa sababu hakuna wa
kuviendeleza vipaji vyao. Kupitia Quran tukufu, tunahitaji kuwabadilisha
wote hawa ili tuwe na jamii imara, inayomjua Mwenyezi Mungu, iliyobora
na inayoishi kwa amani,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JUNI 3, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubary Zubeir (kulia)
na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh
Othman Kaporo (watatu kulia) wakiwa na washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya
Kuhifadhi Qur-aan Tanzania baada ya Waziri Mkuu kuwakabidhi washindi hao
zawadi zao kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni
3, 2018. Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza Ibn Rayizah Hatim Abdullah
wa Saudi Arabia, Mshindi wa pili Hamza Soukouna kutoka Mali na Mshindi
wa tatu Hamzah El- Habashiy kutoka Marekani.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi waliofika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambako Mheshimiwa Waziri Mkuu alikabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania, Juni 3,2018. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Mwenyekiti wa Haj Trust Fund, Sheikh, Swaleh Misky, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt, Mohammed Bilal, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir kabla ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo (kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum (wapili kulia) baada ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment