Monday, May 28, 2018

WAZIRI UMMY AMWAGA FUTARI KWA TAASISI 10 ZA KIDINI NA MAGEREZA JIJINI TANGA

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akimkabidhi futari Mkurugenzi wa Taasisi ya kulea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu ya Goodwill Sayyed Muhdhar Idarus ambapo futari hiyo ambapo taasisi 10 zilipewa futari hiyo kwa kila taasisi ni Unga wa ngano kg 50, mchele kg 100,unga wa ngano kg 50,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20na majani ya chai kilo 3,Maharage Kg 100 na Unga wa Dona Kg 25 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akimkabidhi futari mmoja wa walezi wa vituo vinavyolelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Tanga vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akigawa futari kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali na taasisi za kidini tano zilizopo Jijini Tanga wakiwemo Magereza vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza katika halfa hiyo baada ya 

kuwakabidhi kila taasisi Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
 Sehemu ya wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali Jijini Tanga wakimsikiliza Waziri Ummy Kabla ya kupokea futari
 Ustadhi wa Madrasa ya Zaharau Ustadhi Abduswamad Muhammad akipiga dua kumshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia Futari hiyo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akiwa kwenye Picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali mara baada ya kuwakabidhi Futari
 Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya Futari kwa Taasisi 10 wakiwemo Magareza na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupitia Taasisi yake ya Odo Ummy Foundation leo amegawa futari kwa taasisi za kiislamu na magereza zilizopo Jijini Tanga vyakula mbalimbali ili viweze kuwasaidia wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani. 

Vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi futari hizo mapema leo taasisi zenye wanafunzi waliotika maeneo mbalimbali na wakati mwengine wanakuwa hawana uhakika wa kufutari,watu wengine wajitoleza kulea taasisi hizo pamoja na alisema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria lakini wakikabidhiwa wanaweza kuona namna nzuri ya kuweza kuitumia wakati wa mfungo mtukufu wa ramadhani. 

“Nimeona ni bora nitoe futari hii badala ya kwenda kufuturu kila mahali kwani tutakapofanya hivyo wanaweza kuja wachache na mimi kutokana na kuwa nimetoka kwenye familia ya watu wa kawaida maskini nimeona angalu hicho kidogo ambacho nimejaliwa nitoa kwa taasisi za dini na watoto kwenye mazingira magumu”Alisema. 

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa taassisi za tano zilizo na wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali ambao wamejifunza dini na vituo vinavyolea watoto kwenye mazingira magumu ili wakati huu wa mwezi mtukufu wa ramadhani waweze kutimiza nguo hiyo muhimu ya funga bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile. 

Hata hivyo alitoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kusaidia watoto yatima yanaolelewa kwenye vituo mbalimbali na Taasisi za kidini kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ili waweze kupata uhakika wa kupata mahitaji yao muhimu wakati wa kufuturu. 

Akizungumza baada ya kupokea futari hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwil inayolea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Sayyed Muhdhar alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapatia msaada huo wa futari ambao utakuwa chachu kuweza kuondoa changamoto ambazo wanakabiliana nazo hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani. 

Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri Ummy sio jambo dogo ni kubwa kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hasa kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa ramadhani kutokana na mahitaji kuongezeka. “Namuomba mwenyezi Mungu ampe nguvu na kumjalia maisha marefu na pale alipotoa aweze kuongezewa “Alisema (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments: