MKUU wa mkoa Dodoma,Dk.Binilithi Mahenge amepiga marufuku waajiri wote kutoa ahadi hewa kwa wafanyakazi wanaotangazwa kuwa wafanyakazi bora na badala yake wafanyakazi hao wanatakiwa kupewa zawadi zao na vyeti kadri ilivyopangwa na halmashauri husika au mwajiri.
Mkuu huyo wa mkoa alisema imekuwa desturi waajiri wamekuwa wakitafuta sifa ya kutangaza dau kubwa au zawadi kubwa kwa wafanyakazi waliotangazwa kuwa bora lakini kinyume chake wafanyakazi hao wamekuwa wakiambulia vyeti huku pesa hawapewi na linakuwa deni sugu.
Dk.Mahenge alitoa kalipio hilo baada ya wafanyakazi bora wa jiji la Dodoma pamoja na wafanyakazi bora wa Wilaya ya Chemba kupewa vyeti tu huku wakiahidiwa kupewa fedha baadaye badala ya kupewa fedha muda huo huo.
Akizungumza na wafanyakazi wakati wa utoaji wa vyeti, zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiongozi huyo wa mkoa aliagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Godwin Kunambi pamoja na uongozi wa halmashauri ya Chemba kuhakikisha wanawapatia fedha zao wale wote waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na si vinginevyo.
Alisema imekuwa tabia ya halmashauri nyngi kutangaza wafanyakazi bora na kutangaza kuwapatia vyeti na fedha taslimu lakini hawafanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakizurumiwa au kupewa hundi feki jambo ambalo alisema ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi wanaojibidisha kufanya kazi kwa bidii.
“Haiwezekani wewe mkurugenzi au ofisa utumishi mkaatumia vigezo vyote vya kumpata mtumishi bora mkaandaa vyeti,lakini mkashindwa kuandaa fedha ya huyo mtumishi mnakuja hapa mnatoa ahadi jambo hili siwezi kukubaliana nalo sasa naagiza, mkurugenzi wa Jiji huko wapi?, hata kama hayupo naagiza wafanyakazi wote wanaotakiwa kupatiwa fedha zao wapatiwe le oleo (jana) au kesho kabla ya saa tatu (Leo).
“Imekuwa ni utamaduni wakuwadanganya wafanyakazi kwa kuwaandalia vyeti na kuwatajia zawadi ambazo hawapatiwi hili jambo kwa uongozi wa awamu ya tano hauwezi kukubalika lakini pia kwa sasa Dodoma ni makao makuu hatuwezi kufnya mambo ya aina hiyo hilo ni jambo ambalo haliwezi kukubalika kabisa kila mtu apatiwe haki yake.
DODOMA JIJI/MAKAO MAKUU.
Lcha ya mkoa wa Dodoma kupatiwa adhi ya kuwa makao makuu na manispaa kupandishwa adhi na kuwa Jiji lakini imekuwa tofauti katika sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) kwani hapakuwepo na kiongozi yoyote wa kitaifa.
Katika sherehe hizo zilizopambwa na maandamano mbalimbali hapakuwepo na mkurugenzi wa Jiji, Meya wa Jiji wala waziri yoyote au Naubu waziri na hata mbunge yoyote wa jimbo katika mkoa wa Dodoma.
RISALA YA WAFANYAKAZI
Kwa upande wa wafanyakazi wameitaka serikali kuona uwezekano wa kupandisha mishahara kwa watumishi ili waweze kuendana na hali ya maisha ya sasa kutokana na bidhaa mbalimbali hususani chakula kupanda bei.
Akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Sostenes Ndish, alisema kuwa wafanyakazi wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mishahara midogo ambayo wakati mwingine wafanyakazi wanashindwa kufikia malengo.
Jambo lingine ambalo alilitaja ni pamoja na mafao ya wastaafu kucheleweshwa jambo ambalo alisema seriali inatakiwa kuangalia kwa upya ili inapokaribia mtumishi kustaafu apate fidia yake kwa wakati badala ya kukaa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Ndish alisema kuwa serikali inatakiwa kuwawajibisha waajiri ambao wamekuwa na tabia ya kuchelewesha makato ya watumishi au kutolipa kabisa katika mifuko ya jamii jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa malalamiko kati ya mfuko, mwajiri na mwajiliwa.
Kuhusu sekta binafsi alisema zimekuwa na tabia ya kuwafanyisha kazi watumishi wake lakini wamekuwa hawatoi mikataba wala ajira na kusababisha wafanyakazi wengi kutokuwa na fedha katika mifuko ya jamii jambo ambalo ni hatari kwa utumishi wao.
MAHOJIANO.
MMOJA wa wafanyakazi waliopatiwa zawadi kwa utumishi bara ni pamoja na Dereva wa Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Frank Malecella maarufu kwa jina la Muboss alisema kuwa siri kubwa ya yeye kupatiwa zawadi ya ufanyakazi bora ni pamoja na kufanya kazi kwa utii pamojana kusikiliza mkuu wake wa kaza anasema nini.
“Ili uweze kufanya kazi vizuri ni lazima uwe na heshima kazini, kujali muda wa kazi, kuhusu masuala ya mishahara alisema yeye anakubaliana na kiwango ambacho kimepangwa na serikali huku akiwa na akili ya kujiongeza kwa lengo la kufanya kazi nyngine za kumuongezea kipato” alisema.
Naye Olipa Mwankemwa ambaye ni Ofisa rasilimali watu katika kiwanda cha machinjio ya kisasa ya nyama kilichopo Kizota, alisema kuwa serikali inatakiwa kusimamia zaidi changamoto ambazo wafanyakazi wanakumbana nazo.
Alisema kwamba wafanyakazi wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na mishahara kiduchu,kutokuwepo na usalama wa kutosha katika sehemu za kazi huku akisema kuwa waajiri wengi hawapeleki pesa ya makato katika mifuko ya jamii kwa wakati.
Olipa alisema zipo pia kampuni nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanyisha watu kazi lakini wamekuwa hawapo tayari kuwapatia mikataba ya kazi wala kuwapatia ajira jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kazi.
Kwa upande wake Salum Mkuya ambaye ni mtumishi wa TAMISEMI ,Elimu alisema katatika sherehe za wafanyakazi Mei Mosi kwa wale ambao wanachaguliwa kuwa wafanyakazi bora wanatakiwa kupewa vifaa ambavyo vitawawezesha kufanya mambo ya kimaendeleo.
Alisema yafaa watumishi hao ambao wanachaguliwa kuwa wafanyakazi bora kupatiwa vifaa kama vile vya ujenzi au vifaa vya usafiri kulingana na zawadi ambayo muhusika amekuwa amepangiwa badala ya kuwapatia zawadi kama tv.
Muhsin Mulokozi ambaye ni Ofisa tarafa ya Mlali wilaya ya Kongwa alisema kuwa sherehe za wafanyakazi ni kuwafanya wafanyakazi hao kujitambua na kujitathimini kujua wamefanya kazi kwa kiwango gani kwa mwaka.
Hata hivyo alisema siri kubwa ya kufanya kazi kwa mafanikio ni kuhakikisha mfanyakazi anafanya kazi kwa malengo ya kuwahudumia wananchi pamoja na kujenga uhaminifu kwa serikali na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment