Kundi la Wasanii la Tanga Kwanza likitumbuiza kwenye uzinduzi huo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wanaounda kundi la Tanga Kwanza
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.
Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.
Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.
Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.
“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.
“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.
Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279 zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.
Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.
“Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema tutaendelea kushirikiana”Alisema.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili wananfunzi waweze kuendelea na masomo.
“Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha )
No comments:
Post a Comment