Mchezaji Godfrey Ernest wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom Manyara akimtoka mchezaji wa timu ya Rambo FC pia ya Haydom katika mchezo wao uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom katika Mashindano ya kombe la Kurugenzi Cup 2018 yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo timu ya Rema 1000 FC imeibuka na ushindi wa Magoli 5-3 dhindi ya Rambo FC.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-HAYDOM- MANYARA)
Wachezaji wa timu ya Rema 100 FC ya Haydom wakishingilia mara baada ya mchezaji Raurenc Marco kuifungia timu yake ya Rema 1000 FC goli lao la tano katika mchezo huo uliokuwa mkali dakika zote za mchezo.
Kikosi cha timu ya Rema 1000 FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Rambo FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Rambo FC na timu ya Rema 1000 FC wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Haydom.
Mchezaji Ngaja Junior wa timu ya Rambo FC bukta ya bluu na Masoud Juma wa Rema 1000 FC wakizungumza na waamuzi kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo huo uiofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom.
Baadhi ya watoto wakigawiwa maputo kwenye benchi la ufundi la timu ya Rema 1000 FC.
Kocha wa Rema 1000 FC Jared Ochieng akitoa maelekezo kwa wachezaji wake huku mmiliki wa timu hiyo Bw.Samson Madawa Bora ambaye pia ni Daktari katika Hospitali ya Haydom akimsikiliza wakati wa mapumziko ya mchezo huo.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
Bw. Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na Mawasiliano Halmashauri ya wilaya ya Mbulu akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kuangalia mchezo huo kuhusu huduma ya upasuaji kwa watu walioungua kwa moto inayotolewa na daktari wa kujitolea Joost Binmerts kutoka Uholanzi akishirikiana na madaktai wa Hospitali ya Haydom.
Bw. Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na Mawasiliano Halmashauri ya wilaya ya Mbulu akizungumza na daktari wa kujitolea Joost Binmerts kutoka Uholanzi anayefanya kazi katika Hospitali ya Haydom.
Baadhi ya mashabiki wa mpira waliojitokeza kushuhudia mchezo huo wakifuatilia wakati ulipokuwa ukiendelea.
Baadhi ya mashabiki wakifurahiamoja ya goli lililofungwa katika mchezo huo.
.......................................................................................
Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingi
Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa
kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.
Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho,
upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi,
kwenye mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.
Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na winga
machachari wao Shafii Said wenye dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza
cha mchezo huo.
Mshambuliaji hatari wa timu ya Rema 1000 FC Masudi Juma aliipatia timu
yake bao la pili kwenye dakika ya 29 mara baada ya kuwachambua pasipo
na huruma walinzi watatu wa timu pinzani na kupachika kimiani bao la
kiufundi, hadi mapumziko timu ya Lambo haikuona nyavu ya timu pinzani.
Kipindi cha pili timu ya Lambo FC kupitia kocha wake ilifanya
mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wawili na kuingiza nguvu mpya
ambayo ilibadilisha sura ya mcheo na kuleta maajabu kwenye viwanja
hivyo kwa kurudisha mabao mawili na kuongeza la tatu.
Katika dakika ya 53 mshambuliaji wa timu ya Lambo FC Lazaro Zebedayo,
aliyeingia kipindi cha pili alirejesha matumaini kwa kupachika bao
safi la kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mkabaji
Patrick Zacharia.
Mnamo dakika ya 60 winga machachari wa timu ya Lambo FC Salvatory
Zelote aliachia shuti kali umbali wa mita 23 na kutinga kimiani na
kumuacha kipa ameduwaa hivyo kufunga bao la pili na kusawazisha na
kuwanyanyua mashabiki kwa vifijo na nderemo katika viwanja hivyo.
Timu ya Lambo FC iliamka usingizini baada ya kupata mabao hayo na
kuishambulia kama nyuki timu ya Rema 1000 na kufanikiwa kuandika bao
la tatu kupitia mshambuliaji wao machachari Lazaro Zebedayo ambaye
ndiye mfungaji wa bao la kwanza.
Benchi la ufundi kupitia kocha mkuu wa timu ya Rema 1000 Jerad Ochieng
alifanya mabadiliko ya haraka kwa kumtoa kiungo mmoja na washambuliaji
wawili na kubadilisha sura ya mchezo kwa muda mfupi.
Baada ya mabadiliko hayo, dakika ya 79 kulitokea piga nikupige katika
lango la timu ya Lambo FC na hatimaye mshambuliaji wa timu ya Rema
1000 FC Laurence Marco alizamisha nyavuni mpira uliokuwa ukiambaa
pembeni mwa goli hilo.
Bao la nne la timu ya Rema 1000 FC liliwekwa kimiani na nahodha wa
timu hiyo Shafii Said baada ya kutokea faulu upande wa kushoto na
kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango, kwa mara nyingine tena
dakika mbili baada ya bao la nne kutinga kimiani, mshambuliaji
Lawrence Marco alihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga bao la kichwa
baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Masudi
Juma.
Mara baada ya mchezo kumalizika Mkurugenzi wa timu Rema 1000 Samson
Madawabora hakusita kuonyesha furaha yake katika viwanja hivyo kwa
kuwazawadia kila mchezaji wa timu hiyo shilingi elfu 10,000 papo hapo
uwanjani.
“Timu yetu ipo vizuri kocha wetu Jerad Ochieng ameshawapa maelezo ya
kutosha wachezaji wetu hivi sasa ije timu yeyote tuu sisi sawa
tutawafunga tuu kwani tupo vizuri,” alisema Madawabora.
Wakizungumza mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa timu ya Lambo FC
Paulo Modest alisema kwenye mchezo kuna matokeo matatu kushinda,
kushindwa na kutoka sare hivyo anakubaliana na matokeo hayo huku kocha
wa timu ya Rema 1000 FC Jerad Ochieng akisema wamejiandaa ipasavyo kwa
mpambano ujao.

No comments:
Post a Comment