Tuesday, May 15, 2018

RC KIGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga, amewataka Wakuu wa Wilaya, Watendaji na watushi wa idara ya afya kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Ebola.

Pia pamoja na kuweka uangalizi katika mipaka kuzuia ugonjwa huo usiingie katika mkoa wa kigoma. 

Maagizo hayo aliyatoa jana katika kikao cha kujadili na kupanga mikakati kuhusu njia bora ya kuzuia uingiaji wa ugonjwa wa ebola kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo na Mkoa huo kuwa na muingiliano wa wafanya biashara kutoka nchi hiyo na wengine kwenda kwaajili ya biashara kusababisha ugonjwa huo kuingia kwa urahisi nchini.Amesema hatamvumilia nkuu wa wilaya yeyote au ntumishi wa afya atakae kuwa sababu ya kuingia kwa ugonjwa huo.

Ameongeza kwani mkoa wa Kigoma umekuwa ukiongoza katika magonjwa mengi ya mlipuko kama kipindu pindu ambapo umekuwa ugonjwa mkubwa mkoani humo." Mkuu yeyote ambae wilayani mwake kutabainika kunaugonjwa wa mlipuko atachukuliwa hatua."Wakuu wa wilaya kazi yenu kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi na kuwachukulia hatua watendaji wa afya wasiofanya kazi zao kikamilifu ambao wanasababisha magonjwa hayo kuingia nchini ni wakati wa kuanza kukagua vyoo katika vijiji vyenu," amesema.

Aidha Mkuu huyo amesema hayuko tayari kuona wananchi wanashindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ya milipuko kwani kazi kubwa ya viongozi ni kuwahudumia wananchi.Pia na wananchi wasimamiwe kuweza kuzuia magonjwa ya milipuko na hakuna haja ya Mkoa wa Kigoma kuwa masikini lazima juhudi zifanyike kuhakikisha mkoa unakuwa salama.

Kwa Ofisa Afya Mkoa wa kigoma Kulwa Makono, amesema katika mikakati ya Mkoa wameandaa fedha zitakazotolewa kwa wakuu wa Wilaya kwaajili ya kukagua vyoo katika vijiji na wameleta vyoo ambavyo vinazuia harufu mbaya na kutoka uchafu Nje ya choo wameandaa vyoo zaidi ya 756 kwaaajili ya mashule na vituo vya afya kwaajili ya kuzuia magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Pitter Nsanya kwa niaba ya mganga Mkuu wa Mkoa amesema,ebola ni ugonjwa ambao unasambazwa na virusi vinavyoitwa ebola na ugonjwa huo ulianzia nchini Congo mwaka 1976 na waligundulika wagonjwa 318.Ambapo kati ya hao wagonjwa 248 walipoteza maisha.

Amesema kuna aina tatu za ebola ambazo zinazoambukia kwa ukanda wa Afrika ni Zaire, Sudani na Bundobudi na dalili za ugonjwa huo ni maumivu ya misuli kuharisha , homa kali na kunakuwa na madonda kooni.Pia kupata vipele na kutokwa damu kwenye matundu ya mwili, na ugonjwa huo na dalili hizo huanza kuonekana ndani ya siku mbili hadi siku 21 ambapo hadi sasa idara ya afya haijagundua chanjo wala dawa inayoweza kutumika ilikukomesha ugonjwa huo hayo.

Hata hivyo Nsanya alieleza kuwa tahadhari zinazotakiwa kuchukuliwa ni kuepuka kugusa wanyama, kuepuka kushika majimaji yanayotokana na wagonjwa wa ebola na kuchemsha chakula vizuri.

"Wanyama ndio wanaoweza kuleta shida pamoja na kugusa maiti ya mtu mwenye ebora na katika nchi ya kidemocrasia ya Congo DRC eneo la Ikoko kilomita 30 kutoka Bikoro kumeripotiwa watu 36 waliogundilika na ugonjwa huo na mpaka sasa watu 19 wamepoteza maisha kati yao watatu ni wauguzi wa afya," amesema.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki kwenye mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu  Emanuel Maganga akimkabidhi choo cha Kisasa Mkurugenzi wa Kibondo Juma Mnwele kati ya vyoo 756  kwa niaba ya wakurugenzi wenzake kwa lengo la kuvipeleka mashuleni na katka vituo vya afya  kwa lengo la kuepusha na ugonjwa wa kipindu pindu.

No comments: