Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akisisitiza kuhusu namna idadi ya
watu inavyoongezeka au kupungua wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari
za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bw. Omary Mdoka akiwasilisha mada kuhusu ongezeko la watu
wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa
habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bw. Oscar Mangula akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya
takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za
takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Mariam Kitembe akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada
kuhusu hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hapa nchini kwa
kuzingatia utafiti uliofanyika mwaka 2016/2017 wakati wa mafunzo ya
uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma
leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir akitoa
maelezo kuhusu mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za takwimu
kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mkurugenzi wa shughuli za
kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Irenius Ruyobya
akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa
waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo
ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la
Dodoma leo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
………………
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) imetoa mafunzo ya uandishi wa habari za kitakwimu kwa wanachama wa
chama cha waandishi wa habari Dodoma ili kuwaongezea uwezo wa uandishi
mzuri wa habari za kitakwimu.
Mafunzo hayo ya siku mbili
kuanzia tarehe 26 hadi 27 Mei, mwaka huu yanayofanyika katika ukumbi wa
Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Jijini Dodoma yamefunguliwa na
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa
kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Akifungua mafunzo hayo
Zamaradi Kawawa amesema kutokana na Wizara zote pamoja na baadhi ya
Taasisi kuhamia Dodoma, Dodoma imekuwa ndio kitovu cha shughuli za
Serikali kwa maana hiyo imekuwa chanzo kikuu cha habari zinazohusu
Serikaki nchini hivyo basi majukumu ya vyombo vya habari vilivyopo
mkoani Dodoma yameongezeka na yatazidi kuongezeka kadiri shughuli za
Kiserikali zinavyoongezeka.
“Hapana shaka yeyote kuwa
watumishi wote wa vyombo vya habari vilivyopo Dodoma wanahitaji mafunzo
kama haya kwa ajili ya kuimarisha weledi wao katika kuripoti matukio
mbalimbali yanayotokea mkoani humu,” amesema Zamaradi.
Aidha amesema, maisha ya kila
siku ya mwanadamu yanahusishwa na takwimu hivyo takwimu ni sehemu muhimu
ya maisha ya ulimwengu wa sasa na ndizo zinazotawala namna ya kufikiri
na kufanya maamuzi katika maisha tunayoyaishi.
Ametolea mfano wa ubora wa
maisha ya watu kuwa unapimwa kwa kutumia takwimu, hali ya uchumi, hali
ya biashara, uwekezaji, huduma za usafiri na usafirishaji na hata
michezo. Hivyo basi, uandishi wa habari hauwezi kukwepa matumizi ya
takwimu.
Hata hivyo ametoa wito kwa NBS
kuendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoani ambakk hivi
sasa kuna redio nyingi za kijamii ambazo zinasikilizwa na Watanzania
wengi. Waandishi wa redio hizo wakipata ujuzi wa uandishi wa habari za
kitakwimu itasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kwa upande wake, Meneja wa
Takwimu za Kodi wa NBS Fred Matola amesema matarajio ya NBS baada ya
mafunzo hayo ni kuwa na waandishi wa habari mahiri kwa Jiji la Dodoma
kwa ajili ya kuhabarisha Umma.
“Mafunzo haya yatakuwa tija
kwa waandishi wa Dodoma hivyo kuwanufaisha Watanzania wote kupitia
habari watakazoandika,” amesema Matola.
Nae, Mratibu wa Mafunzo hayo
Said Ameir amesema mafunzo hayo ni ya kipekee, kutokana na Serikali
kuhamia Dodoma na shughuli nyingi za Serikali kufanyika mkoani humo.
Mafunzo hayo ni ya Siku mbili yanashirikisha waandishi wa habari zaidi
ya arobaini kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari.
No comments:
Post a Comment