Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
serikali mkoani Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za kisekta za serikali za mitaa.
Mbali na majukumu hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za mkoa kwa kushirikiana na wakala.
Akizindua kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na kuwajibika ipasavyo.
“Sheria hii inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa “alisema Mghwira.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi Mdogo wa ofisi ya Mkoa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akiitoa katika uzinduzi rasmi wa kamati hiyo.
Wakuu wa wilaya za Siha,Onesmo Buswelu(kushoto) ,Wilaya ya Same Rosemery Senyamule(katikati) na Aron Mbogho wa wilaya ya Mwanga wakiwa katika kikao hicho ambao wao pia ni wajumbe
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa huo.
No comments:
Post a Comment