Saturday, May 12, 2018

JUMIA YATOA SAMSUNG S9 NA S9+ KWA WATEJA WAKE


Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliyoinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mteja Happiness Keto akionesha simu hiyo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia aliyoinunua simu hiyo aina ya Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!
Mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia akionesha simu hiyo kwa wanahabari.


Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mteja Happiness Keto akizungumza kwenye mkutano huo.






JUMIA imekabidhi simu mbili za Samsung Galaxy S9 na S9+ kwa wateja wake wawili ambao waliibuka washindi kupitia zoezi la kusaka simu kwenye mtandao wao (Treasure Hunt) kupitia kampeni ya ‘Mobile Week.’

Katika zoezi hilo wateja waliofanikiwa kuzipata simu hizo zilizofichwa, walipewa ofa ya kuzinunua kwa bei ya chini kupindukia tofauti na gharama yake halisi. Baada ya kufanikiwa kufanikiwa kuipata simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu, wakati mwenzake Lumby Elia yeye aliinunua Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!

Bei halisi ya simu ya Samsung Galaxy S9 ni shilingi 2,049,000 ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,500,000 wakati Samsung Galaxy S9+ ni shilingi 2,315,000 nayo ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,800,000! Hivyo unaweza kujionea ni kwa namna gani wateja hawa walivyokuwa na bahati!

Simu hizi zilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu na kampuni ya Samsung duniani ambapo kwa hapa nchini Tanzania ilikuwa ikipatikana kwa malipo ya kabla kupitia kwenye mtandao wa Jumia pekee.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa simu yake ya Samsung Galaxy S9+, Lumby Elia amesema kuwa ana furaha sana hatimaye kuishika simu hiyo mkononi kwa mara ya kwanza kwani ni kama ndoto kuinunua kwa bei hiyo kwa sababu ni sawa na bure.

“Ni ndoto ya watu wengi kumiliki bidhaa ambayo ni toleo jipya hususani kama simu ambazo kila mwaka huwa zinakuja na matoleo na maboresho tofauti. Simu hii kwangu mimi ni kama ndoto kutokana na ubora na thamani yake pamoja na uwezo ilionao,” alisema na kumalizia Bi. Elia, “Naishukuru sana Jumia kwa zawadi hii lakini pia kwa fursa iliyoitoa kwa wateja wake kuweza kutumia bidhaa halisi na mpya kabisa iliyoingia kwa mara ya kwanza sokoni. Nawasihi wateja wengine wakiona fursa kama hizi wasizipuuzie, ni kweli kama hivi mnavyoona.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott ameongezea kuwa ni madhumuni ya kampuni yake kuona inabadili utamaduni wa Watanzania katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.

“Nafahamu kwamba bado Watanzania wengi wana hofu ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kwa sababu wengi wao wamejaribu kulaghaiwa mara kadhaa walipojaribu kufanya hivyo. Lakini ningependa kuwahakikishia mambo ni tofauti kwa Jumia. Jumia ni sehemu PEKEE inayokuhakikishia bidhaa halisi. Unaweza ukaagiza bidhaa, halafu ukalipia mara baada ya kukufikia, tena ukiwa umeridhika nayo. Hata baada ya kununua bidhaa, halafu ukabadili mawazo yako ndani ya siku 7, ikiwa bado haijafunguliwa wala kutumika, ikakurudishia pesa zako - hata gharama za kusafirisha! Hata namna ya kufikiwa na bidhaa yako ni haraka pia! Inachukua takribani muda wa siku 2 tu kwa bidhaa zinazoagizwa ndani ya jiji la Dar es Salaam,” alifafanua Prescott.

“Kuonesha kwamba tunawajali wateja wetu, Jumia leo inazindua rasmi kampeni nyingine ya ‘Mobile Week.’ Safari hii ikiwa imeboreshwa zaidi kwa ofa, mapunguzo ya bei na zawadi kemkem kwa wateja,” alisema Prescott na kuhitimisha kuwa, “kitu cha kusisimua zaidia, tunafahamu kuwa kwa mashabiki wengi wa mchezo wa mpira wa miguu macho na masikio yote wametega kuelekea kuanza kwa Kombe la Dunia. Jumia hatutowaacha watupu, tuna kampeni kubwa pia itakuja siku si chache pamoja na nyinginezo nyingi zitakazokuwa zikiendeshwa kila wiki.”

No comments: