Sunday, May 20, 2018

DONGOBESH FC YATWAA UBINGWA WA "KURUGENZI CUP 2018" MBULU, YAITANDIKA REMA 1000 FC 3-1

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimkabidhi kombe kapteni wa timu ya Dongobesh FC ya Dongobesh Iddi Podoksi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rema 1000 FC ya Hayodm katika mchezo wa fainali Kombe la Kurugenzi Cup 2018 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom mjini Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Kapteni wa timu ya Dongobesh FC ya Dongobesh Iddi Podoksi akinyanyua kombe juu mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rema 1000 FC ya Haydom katika mchezo wa fainali Kombe la Kurugenzi Cup 2018 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom
Wachezaji wa Dongobesh FC wakifurahia kombe lao mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Rema 1000 FC kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Haydom katika fainali ya Kurugenzi Cup 2018.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akikabidhi jezi kwa timu ya Rema 1000 FC ya Hayodm baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mchezo wa fainali Kombe la Kurugenzi Cup 2018 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom
Mashabiki wa timu ya Dongobesh wakimnyanyua juujuu golikipa wao anayejulikana kwa jina la Mapilau baada ya timu yao kuibuka bingwa wa michuano hiyo na kuibuka kuwa golikipa bora wa michuano hiyo.
Wachezaji wa timu ya Rema 1000 wakiwania mpira wakati mchezo huo ukiendelea.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akipiga mpira golini kuashiria uzinduzi wa fainali hizo.
Kikosi cha timu ya Dongobesh FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Rema 1000 kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya michuano hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akikagua timu ya Dongobesh kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akikagua timu ya Rema 1000 kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza na kumshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi kwa kushiriki kwake katika fainali za michuano hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mchezo huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Haydomtayari kwa kushuhudia mchezo wa fainali uliofanyika leo. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akivishwa skafu na vijana wa chipukizi wakati alipowasili uwanjani hapo kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.
Baadhi ya mashabiki wakiwa wamefurika uwanjani hapo kushuhudia mchezo wa fainali katika ya Dongobesh FC na Rema1000 FC.

No comments: