*Vyandarua Bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona
WAZIRI
Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka
Matangazo katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za
upimaji na Matibu ya Malaria ni bure na Wananchi hawatakiwi kulipia
kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia gharama hizo.
Maagizo
hayo aliyatoa jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati
akizindua ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa
Wakina Mama wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano
wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti
malaria na Shirika la misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea
Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha kwaajili ya
Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure.
Waziri
Mwalimu alisema Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa
pamoja na shirika la JohnsHopkins Center for Communication na
Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID)
kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti malaria Na kuratibiwa na
Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP kwa hiyo vyandarua
hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie.
Aidha
alisema ofisi ya takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha
kupungua kwa kiwango cha Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia
10% kutokana na Mikakati iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza
ugonjwa wa Malaria.
Alisema mikakati ya Serikali ni
kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT)
Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea
vya malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili
kujikinga kuumwa na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu
wakati wa ujauzito ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria.
"Niendelee
Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii
kulipia, wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria
liishe , Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na
namba za simu kwenye vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe
Malalamiko yao ilikuweza kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa
Malaria", alisema Mwalimu.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo
inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na
waliopo ni watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa.
Wakitoa
Malalamiko yao Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo
mbele ya Mh Waziri, Lydia Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi
2500/= kwaajili ya Kipimo cha Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili
ya Matibabu .
Alisema pamoja na kuwa na Kadi ya
bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba Waziri
kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo
elekeza.
Hata hivyo Wananchi hao Shukuru Issa
aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja na
kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na
Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa
maelekezo kwa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa
kituo hicho kwakuwa kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo
cha Afya.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua
bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy
akizungumza leo kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga
mapema leo,mkoani Kigoma.
WAZIRI
Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada
ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda
mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja,
mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa
Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa
Marekani wa kupambana na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania
Andy Karas.
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

No comments:
Post a Comment