Tuesday, April 17, 2018

MPANGO WA ELIMU AFRIKA KULETWA TANZANIA NA PIZZA HUT

Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akiwa na watoto kutoka Shule ya Msingi ya Nzinga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha watoto kusoma na kuandika wa Kiafrika ambapo walipewa boksi nyenkundu zenye vifaa mbalimbali vya kusoma na kuandika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akionyesha vifaa ambavyo vitakuwa kwenye mradi wao mpya uitwao "Red Reading Boxes" kwa ajili ya kuhamasisha watoto kusoma na kuadika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.Mpango wa Pizza Hut wa Elimu wa Afrika Kuletwa Tanzania


Chapa kubwa ya Pizza duniani yabadili boksi zake kuwa boksi nyenkundu za kujisomea kama mradi wake wa kuhamasisha watoto kusoma duniani

KAMPENI mpya inayosafiri ya Pizza Hut Afrika inayohamasisha kusoma kwa watoto imefika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoenda kwa jina la ‘Kipande cha Afrika (Slice of Africa)’ inaongozwa na Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport na timu yake ambayo wanasafiri katika miji 14 na nchi 12 barani Afrika kufuatia mchoro wenye umbo la kipande kikubwa cha chakula aina ya pizza.

“Badala ya kusambaza pizza tunasambaza viboksi vya rangi nyekundu (Red Reading Boxes) tukishirikiana na shirika lisilo la kiserikali ‘READ Educational Trust’, katika kutafuta njia za kivumbuzi za kuendeleza elimu kwa ajili ya watoto katika kila nchi,” alisema Davenport. 

“Kutokana tafiti zinazosema kwamba zaidi ya watoto milioni 280 barani Afrika hawajui kusoma, kampeni hii ni muhimu sana. Elimu na kujisomea ni fursa kubwa katika kuleta maendeleo na tumelenga kutumia ukuaji wa migahawa yetu barani Afrika ili kuleta mabadiliko katika jamii tunazotumikia.”

Katika safari yao timu hiyo ya ‘Slice of Africa’ ikiwa na wafanya biashara wa kampuni hiyo ya Pizza Hut watazindua kampeni ya kujitolea kwa wateja katika kila nchi ili kukusanya fedha zitakazojumuishwa na za kampuni hiyo ili kuweza kusambaza maboksi mengi zaidi.

Katika kila nchi Pizza Hut imechagua shirika lisilo la kiserikali ambalo litafanya kazi ya kutambua walengwa kutoka katika mashirika au shule watakaopatiwa boksi hizo nyekundu. Watoto kutoka shirika la Room to Read wameambatana na timu ya Davenport nchini katika kampeni hii.

“Uwezo wa kusoma katika darasa la nne ukiwa na miaka kumi ni muhimu sana kwasababu kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu unajifunza kusoma na kuanzia darasa la nne hadi 12 ni wakati wa kujifunza,” aliongezea Davenport. “Elimu inaenda nje ya darasa na kuweza kumsaidia mtoto kuwa na ujuzi na kujiamini ili kuweza kushiriki kikamilifu katika jamii. Tunapoona watoto wakifurahia boksi hizi nyekundu ni jambo ni furaha kwetu. Watoto wanapata hamasa ya kusoma na hiyo inatupa matumaini.”

“Shirika la READ linajivunia kuwa mshirika wa kampeni hii inayotupa nafasi ya kuchangia katika lugha na elimu ya mtoto katika bara la Afrika kwa kutengeneza yaliyomo katika boksi hizi nyekundu,” alisema Meneja Mawasiliano wa READ Lizelle Langford. 

“Tukitumia vitu mbalimbali ikiwemo hadithi, michezo ya aina mbalimbali boksi hizi nyekundu zinamhamasisha mtoto anayepokea pamoja na familia nzima na hivyo kuwa njia bunifu ya kukuza lugha ya Kiingereza na ujuzi wa kielimu. Kuwa na vifaa vya kujisomea ni hatua muhimu ya kuelimika zaidi.”

Kampeni hii pia inajenga daraja la kiutamaduni na kilugha kwa kukusanya hadithi katika kila kituo ambazo zote zitaenda kwenye boksi nyekundu ambazo zitasambazwa maeneo mengi Afrika wakati wa Siku ya Elimu duniani mwezi Septemba mwaka huu.

“Tunaamini kuwa kuweza kutoa vifaa vya kujisomea kutaisaidia watu kukua na kutengeneza jamii zenye uwezo zaidi na ni matumaini yetu kila nchi itashirikiana nasi katika hili,” alimalizia Davenport. “Kila senti inayochangwa katika nchi inaenda kwenye kutengeneza boksi hizi nyekundu kwa nchi hiyo. Ni wakati sasa kujiunga na kuwapatia fursa wale watoto wanaohitaji.”

No comments: