Wednesday, April 25, 2018

KITENGO CHA MAGONJWA YA DHARURA MUHAS WAZINDUA KITABU KWA AJILI YA KUFUNDISHIA

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura akipongezwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe na Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura wakimpatia zawadi ya kitabu mmoja ya kiongozi wa wanafunzi hao.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura akitoa shukrani zake wa wanafunzi wake ambao wamekuwa msitari wa mbele kumtia moyo wakati akiandika kitabu chake. Kitabu hicho ni mahususi kwa wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura.
Wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.
Mshehereshaji wa shughuli akitoa machache.
Picha ya pamoja.

Na Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG. 

Jamii imetakiwa kushirikiana vyema na kitengo cha magonjwa ya dharura ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ili waweze kupatiwa huduma iliyo bora. Kauli hiyo ameitoa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe wakati akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa kitengo cha Dharula hafla iliyofanyika ukumbi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Kitengo cha Dharula jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa kitengo cha dharula kwa nchini Tanzania ni kipya sana na kilianza 2010 hivyo kinahitaji maboresho ya mara kwa mara ili kiwahudumie wananchi vyema. 

 "Tunaomba wananchi wawe bega kwa bega na kitengo cha dharula ili kuweza kutoa maoni yao pale wanapoona hawapewi huduma bora, tunahitaji kila mtu awajibike kwa upande wake tusikae kimya kuongelea uchochoroni," alisema Pembe. Aliongeza kuwa kitabu kilichozinduliwa kitaweza kumjenga mwanafunzi awe imara kwa kujua mengi katika utoaji wake wa huduma.

 "Kitabu hiki kimeandikwa na Mtanzania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe na pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura hivyo aliyoyaandika yote ni yale ambayo amekuwa akiyafanya mpaka yakampa cheo hicho kikubwa, naamini hata wanafunzi watakao kisoma vile vile watafuata nyayo zake," alisema. 

 Nae mtunzi mkuu wa kitabu hicho, Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura alisema kuwa wameamua kuandika kitabu hicho ili kuweza kuwasaidia wanafunzi waweze kupata elimu halisi inayoendana na mazingira yetu ya kiafrika. 

 "Katika masomo ya udaktari kuna vitabu vingi kutoka nje ya nchi ambavyo havimsaidii mwanafunzi kwa vile vimeandikwa ili vitumike kwa nchi zilizoendela hivyo vinapofika nchini Tanzania havikidhi kiu ya wanafunzi maana mambo anayokuwa anasoma kama hadithi za kufikirika," alisema. 

Alisema kuwa iko haja ya watunzi wa vitabu wakajikita kuangalia uandishi bora utakaoweza kumsaidia mwanafunzi aweze kujikwamua na si kusoma mambo yakufikirika tu. Kwa upande wake Bingwa wa Magonjwa ya Dharura, Prof. Victor Mwafongo ambaye ni mwalimu wa Dk. Hendry alitoa pongezi kwa kijana wake ambaye anasema nyota yake ameendelea kuwaka kila kukicha kwa kubuni njia mbali mbali za kuwasaidia wanafunzi. 

 "Dk. Hendry ni kijana ambaye walikuwa wanafunzi wangu wa kwanza na leo naona matunda yake kwa kuendelea kung'aa, na kitabu alichokiandika kitawasaidia sana wanafunzi wanaosoma masomo ya dharura," alisema.

No comments: