Kamishna
Msaidizi wa Zimamoto, Hamis Telemkeni (mbele) akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuzima
moto yaliyofanyika kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.
Mkaguzi
Zimamoto Theresia Tengia (kushoto)
na Sajini Maria Gulam (kulia) wakionesha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali
zinazoendesha shughuli zake kwenye Kuiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), moja ya kifaa aina ya blanketi linalosaidia kuzima
na kufunika moto endapo utatokea
bila kumuathiri kwa kuungua.
Sajini
Maria Gulam (mbele) akionesha namna ya kutumia mtungi wa kuzimia moto kwa
washiriki wa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji yaliyofanyika leo kwenye
Kituo cha Zimamoto kilichopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA).
Bi.
Julieth Fonga (kushoto) wa Kampuni ya General Aviation Services iliyopo
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekezwa na
Afisa Usalama wa Zimamoto na Uokoaji, Leonard Chami namna ya kuzima moto
kwa kutumia mtungi, wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo kwenye kituo cha
Zimamoto na Uokoaji cha JNIA.
Afisa
TEHAMA, Bw. Geofrey Youze akifanya zoezi la kuzima moto katika mafunzo
yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Sajini
Maria Gulam leo katika mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika katika
Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), akionesha namba ya kupiga endapo Mwananchi atakuwa
amepata tatizo la moto, ili apate msaada wa haraka.
No comments:
Post a Comment