Sunday, March 25, 2018

WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Na Hamza Temba, Dodoma
..........................................................

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.


Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.


"Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.


Alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3.5 zilitumika.


"Awamu ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017 na utarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimetumika katika awamu hii ya mradi" alisema.


Alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti wa mazao mbalimbali ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati mipya ya kukuza Utalii hapa nchini.


Warsha hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


Naibu Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa warsha hiyo.
 Wajumbe wa Meza Kuu.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
 Baadhi ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Warsha ikiwa inaendelea.

Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments: