Tuesday, March 20, 2018

WAZAZI WAHIMIZWA KUFUATA MAADILI YA MTANZANIA KATIKA MALEZI YA MTOTO


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto kwa kufuata maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.

Imefafanuliwa kuna baadhi ya tamaduni za kigeni wanazoziiga zinachangia kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii zetu .Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Tanzania Gara Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano la kujadili maadili mema na uzalendo kwa ajili ya ustawi wa Arusha yao na Taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Arusha na lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na  viongozi mbalimbali wa Serikali na sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A jijini hapa.

Mheluka amesema wazazi wengi wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata tamaduni za wenzetu wa nchi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa watoto na ya kisasa kitu ambacho si kizuri kwani baadhi ya tamaduni za  wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi zinaporomosho maadili kwa watoto wetu.

“Ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha mtoto nae akathamini tamaduni hizo hizo ujue umempoteza mtoto na umemuaribu kabisa.Unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja.

"Huo si ujanja ni ujinga na ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio vyema.Nikiwauliza wazazi hivi nyie mngelelewa hivyo au mngelelewa vibaya je leo mngekuwepo hapo mlipo?Ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuandaa viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “amesema Mheluka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Arusha Dk.John Palanjo amesema mzazi anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa mtoto wake na mtoto akitakiwa kutimiza wajibu wake kwa mzazi. Ameongeza pia niwajibu wa kila mzazi kumfatilia mtoto wake na kujua maendeleo yake mwenyewe na si kumuachia mwalimu au dada wa kazi amfatilie huku akibainisha mzazi yeyote asitafute mchawi wa mtoto wake kwani mtoto anapokosa naadili.

Amesema asilimia kubwa ya wazazi wao wenyewe ndio wachawi wawatoto wao na kuwashauri wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto wao na kuzungumza nao kipi kibaya na kipi kizuri. " Hii itasaidia kuwawezesha watoto wetu kukuwa kwa kuendana na yale yanayopendeza kwa jamii inayowazunguka

"Mimi na imaini iwapo mzazi akijua wajibu wake hatakubali hata kidogo mtoto wake aharibike ,hivyo ni vizuri mzazi utambue wajibu wako, umrudie Mungu maana ukiwa na hofu ya Mungu lazima utamlea mtoto
kwa kufuata kanuni za kimungu,”amesema. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Arusha Ally Meku  amewataka baadhi ya wazazi kupunguza migogoro ndani ya familia ili watoto nao wasiige tabia mbaya kwani wanapoaanza migogoro katika familia wanashindwa kuwale watoto wao.

Amefafanua na badala yake watoto hao wanaanza kutangatanga hovyo na kuanza kuiga tabia mbaya.
Naibu Katibu Mkuu Wazazi CCM Tanzania bara Godfrey Mheluka akiwahutubia wananchi waliohudhuria kongamano la kujadili 'aadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha.
kamanda wa vijana UVCCM mkoa wa Arusha Philemon Molel maarufu kama Monabani akiongea na wananchi waliohudhuria kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha .
Baadhi ya viongozi  mbalimbali meza kuu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano hilo. 
RTO mkoa wa Arusha Joseph Bukombe nae alikuwepo katika kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wazazi na vijana waliouthuria katika kongamano hilo kufuata maadili ,huku akiwasihi wazazi kuwakumbusha vijana wao kuvaa kofia ngumu wakati wanapoendesha pikipiki zao pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kutokea mara kwa mara
mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo 
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Edmond Rice nao waliuthuria katika kongamano hilo
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Arusha Dkt John Palanjo akizungumza na wananchi waliohudhuria katika kongamano hilo

No comments: