Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga imesema mpaka ifikapo machi 31 mwaka huu, itawachukulia hatua Kali za kisheria wazazi na walezi wote ambao watoto wao wamefaulu na hawajaripoti shuleni mpaka sasa kwa Sababu zisizo na msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Wa wilaya ya Mkuranga wakati akifungua kikao cha bajeti ya mwaka 2018/2019 cha baraza la madiwani kilicho fanyika wilayani humo,na kusema kuwa wanafunzi walioripoti ni 3,439 sawa na asilimia 46 na wanafunzi 217 hawajaripoti mpaka sasa ambao ni sawa na asilimia 5.46.
Aidha amesema mpaka ifikapo march 31 mwaka huu,wazazi na walezi ambao watakuwa hawajatoa taarifa zozote kuhusu sababu za watoto wao kutoripoti shuleni watachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Aidha Sanga amewataka madiwani wote wa wilaya hiyo kushirikiana nae kufuatilia kwa undani suala hilo ili kuhakikisha kuwa wanabaini changamoto zilizopelekea wanafunzi hao kutofika shuleni mpaka sasa."tunachotaka watoto wetu wasome,hatutaki kusukia mtu ameacha shule kwasababu ya kuolewa,wazazi watoe taarifa vinginevyo hatua zitachukuliwa dhidi yao".alisema Sanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Abeid amesema wamepitisha bajeti ya wilaya ya zaidi ya bilion 47 ya 2018/2019 ambayo imekidhi katika katika sekta zote na kipaumbele chao ni kwa mwaka huu ni elimu,afya na maji.
Abeid amesema elimu imepewa kipaumbele kwa sababu wananchi wengi wameitikia wito wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka watoto wao shule hivyo kusababisha utitiri aa wanafunzi hali inayopelekea uhaba Wa vyumba vya madarasa.
Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji Wa wilaya ya Mkuranga Peter Nambunga amesema wao wamelenga sana kwenye elimu na afya kwa sababu na jiografia ya wilaya hiyo pamoja na miundo kutokuwa rafiki hali inayosababisha Mwananchi kutembea umbali mrefu kufuata elimu na huduma ya afya.
Aidha Nambunga ameongeza kuwa katika harakati za kupunguza changamoto za huduma ya wanampango Wa kutafuta mobile clinic ili kuweza kuvifikia vijiji vya pembezoni kama koma na kwale.
Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Mkuranga,Juma Abeid akizungumza na Madiwani wa Wilaya ya Mkuranga katika mkutano wa bajeti ya mwaka 2018/2019.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Diwani wa kata ya Mwanandege,Adroph Kowero akifafanua jambo katika mkutano huo.
Madiwani wakimsikiliza Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Mkuranga,Juma Abeid.
No comments:
Post a Comment