Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
JUMLA ya wanachama 27 kutoka Chama cha NCCR-Mageuzi akiwemo aliewahi kuwa Diwani Kupitia Chama hicho Kata ya Kitagata wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamejiunga CCM.Miongoni mwa hao walijiunga CCM wapo pia wanaotoka Kata ya Nyakitonto na wamefikia uamuzi kutokana na utendaji kazi unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.
Wanachama hao wapya wamejiunga CCM leo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphray Polepole ambaye yupo mkoani Kigoma akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015-2020.Wakizungumzungumza mara baada ya kujiunga na CCM, wachama hao wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kazi inayofanywa na uongozi wa awamu ya tano na viongozi wanavyozunguka kutatua kero za wananchi na kuchochea Maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi.
Damiani Cosmasi ambaye aliwahi kuwa Diwani kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi amesema yeye amekuwa kiongozi katika chama hicho na hajawahi ona viongozi wa chama hicho kufika kuwatembelea na kuwasaidia katika masuala ya maendeleo.Pia amesema wanapowachagua viongozi hawawaoni hadi hapo wanapoanza kuomba kura tena ndipo wananza kuwatembelea.
Amefafani Serikali ya CCM imejitahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliyo ahidi wakati wa kampeni na wameanza kuona mabadiliko na maendeleo mpaka vijijini. "Kila mtu ni lazima amuunge mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia wanyonge ambapo ndicho kilicho kuwa kilio cha wananchi wengi," amesema.
Akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa Shule ya Msingi Kasasa Kijiji cha Kasasa kata ya Kitagata a Wilaya ya Kasulu na wananchi wa Kijiji hicho, Polepole amesema Serikali imeamua kuwasaidia wananchi kuwatoa katika dimbwi la umasikini na kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule na wanafunzi wote wanaofikia umri wa kwenda shule waende kama Ilani ya CCM inavyoeleza.
Amesema kwa kazi kubwa inayofanywa na CCM na Serikali hiyo ni lazima wananchi wakubaliane nae kwakuwa anachokifanya ndilo lililokuwa hitaji la wananchi wengi."Na Serikali imeandaa fedha nyingi kwaajili ya kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikikisha wanaondokana na umasikini kupitia miradi ya maendeleo inayoanzishwa na Serikali ya CCM.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kitagata Sabasi Matabura amesema shule hiyo imeanzwa kujengwa kwa nguvu za wananchi na mchango wa wananchi Sh. milioni 11 na fedha hizo zimetolewa baada ya wananchi hao kuchoshwa na kero ya wanafunzi wao kutembea umbali mrefu kufuata shule sehemu iliko.Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa kushilikiana na Serikali wameahidi kutoa kiasi cha Sh. milioni 40 Kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Shule hiyo.
Ameongeza na ujenzi huo utakamilika mwaka 2019 na wanafunzi waanze kupata elimu karibu na maeneo yao wanakoishi na kuepukana na changamoto hiyo.Katika ziara yake wilayani Kasulu Polepole ameshiriki ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mvugwe, uwekaji zege katika Shule ya Msingi Kasasa na kutembelea wanufaika wa mfuko wa TASAF pamoja na kutembelea kiwanda cha Uchakataji wa Muhogo katika Kijiji cha Nyamidaho.
Pia ameahidi kupeleka Sh.milioni 50 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wajasiliamali.
No comments:
Post a Comment