Saturday, March 3, 2018

MSIUZE UFUTA WENU MASHAMBANI PELEKENI MINADANI-MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akisalimiana na Diwani wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,5 2018
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na mzee Omar Issa, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,
Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee Omar Issa kulia na mzee Mussa Lambamba katikati, katika Kata ya Narungombe, Wilayani Ruangwa, Suleiman Likuche Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni, katikati ni mzee Mussa Lambamba. Machi,5 2018,.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa ufuta katika mikoa inayolima zao hilo nchini kuuza kwa kutumia njia ya minada na si mashambani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Machi 03, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Nachihungo, Narungombe na Chikwale.Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi amesema ili wakulima waweze kupata tija ni vema wakauza ufuta wao kwa kupitia minada kama inavyofanyika katika zao la korosho

“Usikubali kumuuzia mtu yeyote ufuta wako ukiwa shambani kwa sababu bei atakayonunulia ni ndogo kulinganisha na soko, naamini ufuta wote ukiuzwa katika minada mtaona faida.”Kufuatia agizo hilo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue aandae utaratibu wa maeneo ya kukusanyia ufuta na kufanyia minada.

Amesema ufuta unaolimwa nchini ni bora na unapendwa sana duniani hivyo wasiwe na wasiwasi. Baadhi ya Mikoa inayolima ufuta kwa wingi ni Lindi, Pwani, Dodoma, Manyara, Kigoma na Singida.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema vijiji vote visivyokuwa na umeme nchini vikiwemo vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa katika REA awamu ya tatu.

Amesema wananchi waendelee kuwa na subira kwa sababu tayari mkandarasi ameshaanza kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji vingine vya wilaya hiyo na atafika kwenye maeneo yao.Alibainisha kuwa mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wote nchini waunganishiwa nishati ya umeme kwenye majumba yao, hivyo waendelee kuwa na subira na kushirikiana na Serikali yao.
 
Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama alisema, “Huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji”.

Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kote nchini kutunza vyanzo vya maji ili kuliepusha taifa kugeuka jangwa pia miradi inayoletwa na Serikali iwe endelevu

No comments: