Waziri Lukuvi akutana na wananchi waliokabidiwa hati zao
Na Mwandishi wetu, Globu ya jamii.
MSANII
wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda
mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa
wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali,
kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya
Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme - LTSP).
Programu
hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi
mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi ili kukabiliana na migogoro
ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini
Tanzania.
Programu
hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo
takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na
kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero
na Ulanga.
Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.
Mpoto
ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma
mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili
anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia
kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na
wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la programu ya
Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme - LTSP).
Mshairi
huyo amesema baada ya kuzungumza na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa
na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada
ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao
(viwanja na mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.
“Kwa
miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na
mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana
nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme
(LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi
baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho
Mpoto.
“Binafsi
kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na
wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii
programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii
programu. Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika
harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata
fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro
wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii
programu inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila
kipande cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki,
naamini itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania,
hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.
Alisema
bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya
kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo
mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada
atawasiliana wahusika kwaajili ya kutatua kero za wananchi.
Kazi
nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na kusimika
alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za Kilombero,
Ulanga, Malinyi na Mufindi, Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua
migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti
vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi
ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa
masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.
Viongozi
wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa
Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu
iko katika Wilaya zao.
Hivi
karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa
na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu hiyo na
kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima
ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula
nae alifanya ziara katika eneo la programu.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi akikabidhi hati
kwa mmoja wazee waliofanikiwa kumilikishwa ardhi.
No comments:
Post a Comment