Monday, March 5, 2018

Manispaa ya Ilala yapitisha bajeti ya sh. bilioni 287

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BARAZA la Madiwani Manispaa ya Ilala imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Mwanduga amesema kuwa fedha hizo zitapatikana katika makundi mawili ya ruzuku pamoja na vyanzo vya ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa katika bajeti hiyo.

Amesema kuwa chanzo cha mapato ya ndani ni wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha nyingine zitakuwa ni za ruzuku.Mwanduga amesema kuwa kila diwani anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa manispaa.

Amesema kuwa bajeti hiyo itatekelezeka ni pamoja na kuwa na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato ya ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza miradi.

Aidha amesema kuwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa manispaa imethubu ikiwa ni pamoja na kujenga shule nne pamoja na kufanya ukarabati kwa bajeti iliyoishia 2018.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Anatoglo 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Ando Mwankuga akiwaeleza Madiwani jinsi mipango na miradi ya Maendeleo katika kata ya Segera itakavyoendeshwa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akiwasilisha makadilio ya bajeti ya Mwaka 2018/ 2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kissi akichangia jambo katika bajeti hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji Mshamu Kassim akiwasilisha makadirio ya bajeti katika kamati yake.
Wabunge wa jimbo la Ilala na Segerea , Azzan Zungu na Bonnah Kaluwa wakisoma kwa makini makblasha ya bajeti ya Manispaa ya Ilala.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara akichangia mada katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani.
Diwani wa Viti Maalum kata ya Buguruni , Husna Masoud akichangia jambo katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani
Madiwani Manispaa ya ilala wakiendelea na kikao cha Bjeti ya Manispaa hiyo katika ukumbi wa Anatoglo Dar es Salaam. 

No comments: