Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam limepitisha makadirio ya mapato kwa mwaka 2018/2019
Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo kwa Mwaka 2018/2019 imekadiria kutumia fedha Sh.
98,238,193,600 ambapo katika fedha hizo Sh. 76,607,163,700 ni matumizi
ya kawaida na mishahara ambayo sawa na asilimia 78 ya Bajeti yote
Wakati Sh 21,631,029,900 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo sawa na asilimia 22 ya bajeti yote.
Akizungumzia
makadirio hayo Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob
amesena wamekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato ya
ndani katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambayo ni
Sh.12,600,760,400.00 na Sh. 8,498,717,600 sawa na asilimia 40 zimetengwa
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na nishahara.
Akifafanu zaidi wakati anasoma bajeti hiyo Jacob amesoma vipaumbele 17 vya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019
Ametaja
vipaumbele hivyo ni ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Sh bilioni 3, uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya
ndani,kukusanya Sh.bilioni 25.7
Pia
miradi ya maendeleo imetengewa fedha kiasi cha Sh.billioni 21.6 wakati
kipaumbele cha nne kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua dawa
na vifaa tiba Sh.bilioni 8.2.
Jacob
ametaja kipaumbele cha tano ni kupandisha maslahi ya wajumbe Serikali
za Mitaa kutoka sh. 5000 kwa mwezi mpaka sh 20,000 kwa mwezi.
Pia
kuboresha miundombinu ya barabara kwa viwango vya lami,matengenezo ya
kawaida,kujenga madaraja na makalvati na vivuko vya waenda kwa miguu,
fedha kiasi cha Sh.bilioni 1.4 zimetengwa kupelekwa TARURA.
Jacob
amesena kipaumbele cha saba ni uenzi wa viwanda vidogovidogo na
uwekezaji,fedha kiasi cha Sh.billioni 1.2 zimetengwa kuanzisha viwanda
vidogovidogo.
Pia mikopo ya Wanawake,Vijana na walemavu,kiasi cha fedha Sh.Billioni 1.14 zimetengwa.
Ameongeza pia ukarabati wa Viwanja viwili vya Michezo na Uanzishwaji wa Meya Cup,Kiasi cha fedha Sh milioni 150 zimetengwa.
Wakati
ununuzi wa magari na mitambo ya kisasa ya kuzolea taka na kusafisha
Halmashauri ambapo kiasi cha Sh. bilioni 1.2 zimetengwa.
Jocob
ametaja kipaumbele kingine ni ujenzi wa Ofisi za walimu kwa shule za
sekondary na Msingi,Kiasi cha Sh.milioni 300 zimetengwa.
Pia
kipaumbele cha 11 ni kuboresha huduma za usambazaji wa maji safi na
salama kwa wananchi,maeneo ya kwembe,kibamba,Goba,kimara,saranga,Mbezi
na Msigani fedha Kiasi cha Sh.bilioni 1.303 zimetengwa kumaliza tatizo
la Maji Ubungo.
Jacob
amesema huduma za afya bure kwa wazee na upewaji wa Vitambulisho kwa
ajili ya matibabu. Fedha kiasi cha Sh.milioni 60 zimetengwa.
Amesema
kipaumbele cha 14 ni kuboresha huduma za ushauri na ugani kwa ufugaji
na kilimo cha mjini,fedha kiasi cha Sh.milioni 120 zimetengwa.
Kipaumbele
kingine ni uanzishwaji wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ubungo,fedha
kiasi cha Sh.milioni 100 kwa ajili ya utwaaji wa eneo la Hospitali na
upembuzi yakinifu.
Jacob amesema pia uanzishwaji wa machinjio ya kisasa ya Nyama Halamshauri ya Ubungo,fedha kiasi cha Sh.milioni 150 zimetengwa.
Wakati
kipaunbele cha 17,Jacob amesema ni uanzishwaji wa ujenzi wa masoko
makubwa ya vyakula na Nafaka, Kibamba na Kwembe fedha kiasi cha Sh
Milioni 450 ambazo zimetengwa.
"Kwa
pamoja tujenge Halmashauri yetu kwa maslahi ya wananchi
wetu,tutaendelea kusimamia maendeleo ya wananchi kwa kuhakikisha
vipaumbele vyetu vinatekelezwa," amesema Jacob.
No comments:
Post a Comment