Tuesday, March 27, 2018

DKT KALEMANI ATOA MAAGIZO WAKANDARASI WA REA NCHINI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii ch a Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Y ona Mark na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuluni Selemani Omari
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akiteta jambo mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumban i Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisalimiana na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji ni awamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waataalamu mbalimbali wanaotekeleza mradi wa rea awamu ya tatu mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo
Ssehemu ya wakandarasi wakifuatilia uzinduzi huo



WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wa wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu. 

Dkt Kalemani aliyasema hayo leo wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga. 

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo,Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo .

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema. 

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto ya wananchi kutapeliwa na mafundi ambao wamekuwa wakiwabambikia bei kuwaambia walipe kidogo kabla ya kulipia 27000 ambazo wanapaswa kulipa jambo ambalo ametaka likomeshwe haraka. 

“Mameneja, Wakandarasi tuna changamoto wananchi kutapeliwa kuna tabia imezuka mafundi wanawabambikia bei wanaawaambia walipe kidogo kabla ya kulipa elfu 27000 labda niwaambie tu kwamba mtu wa namna hiyo atakayepatikana watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria”Alisema Waziri huyo. 

Alisema mradi huo utakwenda kila kijiji, kitongoji na nyumba kwa nyumba huku akieleza hata kama nyumba unayokaa utaona hakuna sehemu ya kutundukia waya weka hata kwenye mti ili mradi uweze kufikiwa na huduma hiyo. 

Aidha alisema kusudio lingine ambalo alilojia ni kuweka msukumo kwa wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana ili kuweza kumaliza mradi huo kwa wakati ili walengwa waweze kunufaika nao. Waziri huyo pia aliwataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme ikiwemo Transfoma kwa kuhakikisha kutokuiba mafuta kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo. 

“Ndugu zangu tukishirikiana kuilinda miudombinu ya umeme kwani serikali inatumia gharama kubwa kuifikisha kwenye maeneo yenu lakini pia Diwani wa Kata hii anzeni kutenga fedha kwa ajili ya kuunganisha kwenye taasisi za umma kwenye maeneo yenu”Alisema(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments: