Saturday, March 10, 2018

ASASI YA KIRAIA YA FEDHA KUJA NA MRADI WA “VIJANA NA ELIMU YA PESA” (VIEPE)

 Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kutambulisha mradi wa "Viepe" kwa kutoa elimu kwa vijana wa sekondari kakika mkoa wa Dar es Salaam na baadae Tanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa FEDHA, Mohamed Mchoro na kushoto ni  Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei. 

ASASI ya kiraia ya Financial Education for Development and human Achievement (FEDHA) Machi 28 mwaka huu kuzindua mradi wake juu ya kuelimisha vijana kuhusu udhibiti sahihi wa pesa binafsi katika nyanja za utafutaji na utumiaji pesa, uwekaji akiba, uandaaji wa bajeti na uwekezaji wa pesa ili kuwawezesha kukuza ustawi wao wa kipesa na kufikia uhuru wa kifedha.

Hayo ameyasema Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa 

Akizungumza kuhusu asasi ya FEDHA, Bw. Jafari Selemani – Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo amesema “Asasi ya kiraia ya FEDHA ni asasi pekee ambayo imejikita katika utoaji wa elimu ya udhibiti pesa binafsi ili 
kukuza uelewa wa masuala ya kifedha kwa umma wa watanzania kuanzia ngazi ya chini yaani wakiwemo watoto, vijana hadi watu wazima, dhima yetu ni kuwafanya watanzania wapate ujuzi,weledi na taarifa sahihi 
juu ya masuala ya kifedha ambapo itawasaidi kufanya maamuzi ya kujiamini yenye manuufaa kwao binafsi na kwa nchi katika kuhakikisha tunapata sekta ya fedha na uchumi imara na endelevu”

“Malengo ya FEDHA ni, kukuza ustawi wa 
kipesa kwa kutoa elimu; kuwezesha watanzania kutambua wajibu na haki zao kama watumia wa bidhaa na huduma za kifedha; kushiriki kuleta ujumuishi wa uchumi na kifedha Tanzania; na Kushirikiana na wadau 
mbalimbali katika kupambana na Umasikini pamoja na udhibiti finyu wa rasilimali fedha.” amesema Selemani.

Kwaupande wake Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei amesema  kuwa,”Mradi wa Vijana na Elimu ya Pesa ni mradi ambao unalenga kuongeza weledi, ujuzi na uwezo wa vijana juu ya udhibiti na matumizi 
mazuri ya pesa, mradi umelenga vijana hasa wa Elimu ya sekondari.

Vijana ndio muhimili,injini na nguvu kazi ya kuleta maegeuzi ya kiuchumi na hususani tukiwa katika kufanikisha sera ya Tanzania ya viwanda, kwahiyo elimu ya pesa binafsi ni msingi madhubuti kwa uchumi wetu.

Ametoa rai kwa wadau mbalimbali wakiwemo, Serikali kupitia wizara na taasisi zake kama wizara ya fedha na uchumi, wizara ya ajira vijana na kazi, wizara ya elimu, DSE, TIRA, TIC, TIB na  SSRA kuwaunga mkono na 
kuwapa ushirikiano ili waweze kuwafikia vijana na watanzania wengi.

No comments: