Monday, February 5, 2018

WAZIRI KIGWANGALLAH AWASHUKIA VIONGOZI WANAOTAKA KUFUTWA KWA MAENEO YA HIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza ) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa tatu ) wakiruka viunzi wakati walipotembelea jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu ambao alikutana nao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha tatu cha kamati hiyo kilichofanyika jana mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (katikati) wakipatiwa maelezo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa, Wilberd Mtongani ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa tatu kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama (wa kwanza kushoto) wakipatiwa maelezo na Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Iringa, Wicliph Benda ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Naibu Waziri wa Wizara Japhet Hasunga ( wa kwanza ) akiwa ameambtana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakiruka viunzi wakati alipotembelea jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa tatu kushoto) wakioneshwa ramani ya eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa Wilberd Mtongani ( wa kwanza kulia) wakati 2 walipotembelea eneo hilo kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha ili kujenga mji mpya wa kitalii mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza kulia ) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( katika ) wakati walipotembelea jana eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kuhaulishwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu ambapo Waziri Kigwangallah anakutana nao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu wakimsikiliza Waziri Kigwangallah katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama akitoa neno la shukrani kwa viongozi kwa niaba ya Wajumbe wa kamati hiyo katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza kulia ) akiwa ameambatana na wataalam wakati alipotembelea jana eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kuhaulishwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ( wa pili kushoto) akiwa ameambatana na baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wataalamu kutoka mkoani wakitembea kuangalia mipaka ya eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa huo kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika eneo hilo. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT).

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangallah amesema kuwa hatajibu maombi yoyote yaliyowasilishwa ofisini kwake kutoka kwa  Wakuu wa mikoa, Halmashauri pamoja na  Wakuu wa wilaya  ya kufuta maeneo ya Hifadhi ili maeneo hayo yaweze kutumika Kwa ajili ya  matumizi mengine.

Amesema kuwa maeneo hayo yalitengwa kisheria na yana umuhimu mkubwa kiuchumi na kijamii hivyo lazima yaendelee kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho. Amesema katika kipindi  cha Uwaziri wake hatajibu ombi lolote lile linalohusu kubadili matumizi ya maeneo hayo kwa vile kuwa na misitu sehemu za mijini ni sehemu ya maendeleo.

Aliyasema hayo jana mjini Iringa wakati alipokuwa akizungumza kwa mara ya kwanza na kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu iliyokutana kwa ajili ya kufanya kikao chake cha tatu tangu ilipoundwa mwaka jana ikiwa pamoja na kutembelea msitu wa Hifadhi wa kihesa Kilolo uliiombwa na uongozi wa mkoa kufutwa ili upate kutumika kwa kuweka miundo mbinu mipya ya mji wa kitalii.

Katika kikao hicho ambacho Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alishiriki, Waziri Kigwangallah  alimuomba Mkuu huyo awafikishe ujumbe Wakuu wa mikoa wengine  ambao walituma na wanaotarajia kutuma maombi ya namna hiyo kuwa yeye  hatakaa ayajibu hadi pale  tu yule  aliyemteua ampe maelekezo na si vinginevyo"

Amesema kuwa  Halmashauri nyingi nchini kila zikiona maeneo ya Hifadhi zimekuwa zikifikiria kubadili matumizi ya maeneo hayo ili yatumike kwa shughuli zingine za maendeleo kama vile kupima viwanja ili kuwauzia wananchi kwa lengo la kukusanya mapato.

"Ofisin kwangu kuna maombi mengi mno ambayo hata sielewi nianze na lipi na niache lipi, nasema sitajibu ombi lolote lile" alisisitiza Waziri Kigwangallah. Aidha, Waziri Kigwangallah mara baada ya kuzungumza na kamati hiyo alitembelea eneo la hifadhi ya msitu huo huku akiwa ameongoza na kamati hiyo pamoja na Uongozi wa Mkoa wa huo .

Katika kutembelea eneo hilo, Waziri Kigwagwallah aliwashukia viongozi wa Halmashauri kwa kuanzisha dampo katika eneo hilo huku kamati ikijionea magari matatu ya taka yakiendelea kumwaga uchafu kwenye eneo hilo jambo ambalo ni kinyume na sheria za uhifadhi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga  aliwashukia watendaji wa mkoa huo wakati walipokuwa wakipishana kutoa maelezo kuhusiana na mipaka na matumizi ya eneo hilo endapo Wizara itaridhia ombi lao la kubadili matumizi ya eneo hilo.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alimuhakikishia Waziri kuwa eneo hilo endapo watapewa litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. Waziri Kigwangallah mara baada ya kutembelea eneo hilo wakati akitoa majumuisho yake, Alisema kuwa kufuatia ziara hiyo anasubili ushauri utakaotolewa na kamati ya kitaifa ya msitu ndipo atakapokuwa na jibu kuhusiana na ombi la kubadilia matumizi la eneo hilo .

Pia, Waziri Kigwangallah aliiagiza ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa maeneo ya milima kwa vile sio moja ya maeneo ya hifadhi  yaongezwe katika eneo la hilo lengo likiwa ni kuzuia uharibifu wa uoto wa asili unaoendelea katika maeneo hayo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati akitoa neno la shukrani alimhakikishia Waziri kuwa watamshauri jambo lolote lile  linalohusu misitu bila kujali litamfurahisha au litamuudhi, kitakachoangaliwa hapo ni maslahi mapana ya taifa.

Katika hatua nyingine ,Waziri Kigwangallah  ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu nchini  (TFS) kuanza kuweka nguvu nyingi katika kuhifadhi misitu baadala ya kuvuna na kufanya biashara ya mazao ya misitu. Alisema licha ya kuwa TFS imekuwa ikifanya vizuri katika baadhi ya maeneo  lakini katika suala la kuhifadhi misitu imekuwa kama vile  sio kazi yake " yenyewe kazi yake imekuwa ni kuvuna kilichopandwa, kuuza na kukusanya mapato yatokanayo na mazao ya misitu" alisema. 

Wakati huo huo, Waziri Kigwangallah amesema Wizara inakusudia kuchukua misitu yote iliyo chini ya vijiji na Halmashauri kwa vile zimeshindwa kuisimamia ipasavyo na hivyo kupelekea sehemu kubwa ya nchi kugeuka kuwa jangwa.

Mbali na hilo amewaonya wananchi wanaowazuia watendaji  kuweka vigingi katika mipaka ya hifadhi, huku wengine wamekuwa wakivingoa na wengine kuhamisha vigingi hivyo kutoka eneo moja hadi jingine kuwa  waache tabia hiyo moja la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

No comments: