Monday, February 5, 2018

Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mkoani Manyara

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo mbele ya mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa (katikati) mara baada ya kuwasilia katika Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Mama Fissoo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu. Kutoa kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage na Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa wa Mkoa Kennedy Kaganda.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akizungumza jambo alipokutana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) leo Ofisini kwake mjini Babati, Mkoani Manyara. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akisoma kwa makini nakala za Sheria ya Filamu na Kanuni zake mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) Ofisini kwake leo mjini Babati. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.




Kutoka Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa WA Mkoa wa Manyara Kennedy Kaganda na Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage wakifuatilia mazungumzo baina ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa (hawapo pichani) walipokutana ofisi kwa RAS –Manyara, mjini Babati leo.Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Babati
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Katibu huyo yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu katika mkoa huo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa.


Na: Frank Shija – MAELEZO, Babati,


Wawekezaji wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa Manyara badala ya kukimbilia katika maeneo ambayo yamezoeleka na wadau wengi wa maendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo Mjini Babati na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara alipokuta na ujumbe kutoka Bodi ya Filamu Tanzania ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo mape hii leo.

Kaimu Katibu Tawala huyo ameema kuwa Mkoa wa Manyara unazo fursa nyingi za uwekezaji hivyo ni vyema sasa wawekezaji wakatumia fursa hizo na kuja kuwekeza katika Nyanja tofautitofauti za uwekezaji ikiwemo kilimo, viwanda na ufugaji.

“ Mkoa wetu wa Manyara unazo fursa nyingi ambazo kama wawekezaji wakijitokeza watanufaika nazo, hivyo ni wito wangu kwao kuwa waje mkoani Manyara watumie fursa hizo, tunayo maeneo yakutosha kwa shughuli za uwekezaji”, alisema Kaimu Katibu Tawala huyo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa maeneo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu nchini hasa zinazohusisha wageni kutoka nje ya nchi.

Aliongeza kuwa kitu kikubwa kinachoubeba mkoa huo ni mandhara na jiografia ya ambayo imekuwa kivutio kikubwa katika uwekezaji hasa katika eneo la utalii na filamu hapa nchini.

“ Ni jambo muhimu Mkoa wa Manyara mkajivunia kuwa na mandhari inayovutia wawekezaji, katika tasnia ya filamu wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wanakuja na kuhitaji kutumia mandhari ya Wilaya ya Mbuli katika uandaaji wa filamu zao hiyo ni moja ya fursa muhimu ambayo pia itatumika kuutangaza zaidi mkoa wenu”, alisema Bibi. Fissoo.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu majukumu ya Bodi hizo na zinazoongozwa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya.

No comments: