Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAAJIRI
wa kampuni nne tofauti wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa kadhaa yakiwemo ya
kushindwa kujisajili na kuwasilisha taarifa za shughuli wanazozifanya
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi [WCF].
Washtakiwa
hao, Malakkara Semis na Shafeek M. Purayil ni Wakurugenzi Watendaji wa
Kampuni ya SPASH INTENATIONAL CO. LTD. Silas Shemdoe na Deusdedit
Samwel Kibassa ambao ni Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya ENCC
CONSULTANTS.
Wengine
ni Wakurugenzi Watendaji wa LASAR LOGISTIC, Abshir Farah Gure na
Farhiya Hersiwarsame, wakati Mshtakiwa mwingine ni Josephat Alexander
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KAMANDA SECURITY GUARDS CO.
LTD.
Washtakiwa
wamesomewa mashtaka yao na waendesha mashtaka tofauti wa Serikali
wakiongozwa na Wakili wa Serikali Emilly Kiria mbele ya Hakimu Mfawidhi
Victoria Nongwa. Wanashtakiwa kinyume cha Kifungu cha 71 (1) (a) na 71
(4) cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi Sura ya 263 marejeo ya mwaka
2015.
Akisoma
mashtaka yanayomkabili Joseph inadaiwa Januari, mwaka 2018 walishindwa
kujisajili na kutoa taarifa muhimu za shughuli zake na za wafanyakazi
kwa Ofisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Ilidaiwa
Januari 11, mwaka 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kutoa taarifa mihimu
za waajiriwa wake ikiwamo majina na mishahara ya wafanyakazi.
Katika
kesi ya jinai namba 33 ya mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Benson Mangowi alidai washtakiwa Malakhara Semis na Shafeek Purayil
wa kampuni ya Spash International Co.Ltd Desemba 25,mwaka 2017
walishindwa kusajili na kutoka taarifa muhimu za shughuli za kampuni kwa
Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Pia
walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi wao kwa Ofisa
aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF ambapo Septemba 6,mwaka 2017
washtakiwa hao walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi ikiwamo
majina na mishahara.
Wakati kesi hiyo ikisomwa Malakhara hakuwapo mahakamani.
Katika
kesi nyingine, wakili wa Serikali, Emma Msofe amedai washtakiwa Abshir
Gure na Farhiya Warsame wa kampuni ya Lasar Logistic Limited,
walishindwa kusajili na kupeleka taarifa muhimu kwa Mfuko wa WCF.
Alidai
kuwa Oktoba 19,mwaka 2017 walishindwa kutoa taarifa muhimu zikiwamo
majina na mishahara. Pia wanadaiwa Novemba 27,mwaka 2017 walishindwa
kupelekwa taarifa za mfanyakazi wao, Lihikambo Yunus ikiwamo
kitambulisho cha Taifa, cha mpiga kura, leseni, mkataba wa ajira,
taarifa za msharaha na taarifa ya polisi kwa afisa wa mfuko wa WCF.
Wakati kesi hiyo ikisomwa Abshir alikuwapo mahakamani lakini Farhiya hakuwapo.
Katika
kesi namba 35,mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi Derrick
Mukabatunzi alisisimama mahakamani hapo na Kuwaita washtakiwa Riziki
Shemdoe na Deusdedit Kibassa ambapo wakili huyo aliiambia mahakama kuwa
mshtakiwa mmoja hakuweza kumpata na kwamba mwingine alikuwa akiuguliwa
na mkewe Dodoma.
Hata hivyo, Mahakama imetoa hati za wito za Kuwataka mahakamani washtakiwa hao.
Washtakiwa wote wamekana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika.
Hakimu
Nongwa alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo kila
mdhamini atasaini ahadi ya Sh 50 milioni, washtakiwa wote, wako nje kwa
dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Februari 22,mwaka 2018 ambapo washtakiwa
hao watasomewa maelezo ya awali (PH).
Akizungumza
nje ya Mahakama Mwanasheria wa WCF, Deo Victor alisema kabla ya Mfuko
huo kuchukua hatua hii ya kuwafikisha mahakamani, washtakiwa walipewa
taarifa ya kutekeleza takwa hilo la kisheria katika tarehe mbalimbali,
kati ya Septemba 2017 hadi Januari mwaka 2018 lakini walishindwa
kutekeleza.
Wakurugenzi
Watendaji wa Kampuni ya Spash International Co Ltd Shafeek Purayil
(kulia) na Japhet Alexander wa Kampuni ya Kamanda Security Guard Co.
Ltd, wakipelekwa mahabusu ya Mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo
Februari 19, 2018 baada ya kusomewa mashtaka mawili ya jinai kwa
kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na
kuwasilisha taarifa za shughuli za Makampuni wanayoyaongoza kwa Mfuko
huo. Washtakiwa wakipatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo
kisichopungua miaka mitano (5), jela au faini isiyozidi shilingi milioni
hamsini au vyote kwa pamoja.
Shafeek
Purayil(mbele) na Japhet Alexander wakitoka mahakamani baada ya
kusomewa mashtaka na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bibi Victoria
Nongwa.
Shafeek Purayil
Meneja
Matekelezo (Compliance Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,
(WCF), Bw. Victor Luvena akizungumza na waandishi wa habari nje ya
mahakama hiyo. Alisema washtakiwa wengine Zaidi watapandishwa kizimbani
Jumanne Februari 20, 2018 kwa makosa hayo hayo. Kulia ni Mwanasheria wa
WCF, Bw. Deo Ngowi.
Meneja Matekelezo (Compliance Manager), wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Victor Luvena akizungumza na
waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo. Alisema washtakiwa wengine
Zaidi watapandishwa kizimbani Jumanne Februari 20, 2018 kwa makosa hayo
hayo.
No comments:
Post a Comment