Saturday, February 3, 2018

VULLU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI NYUMBA YA MGANGA, ZAHANATI YA KIJIJI CHA KOMA

KAIMU mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo akimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu (kushoto aliyesimama)kwa kuchangia baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 vilivyogharimu zaidi ya mil.1.6
MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu, akimkabidhi kaimu mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo (mwenye gauni la kitenge) baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 alivyochangia ambapo vimegharimu zaidi ya mil.1.6.Picha na Mwamvua Mwinyi
 
………………

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga.

MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani,Zainab Vullu amekabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji pamoja na malumalu vipande 500 ,vilivyogharimu sh .milioni 1.6 ,katika halmashauri ya Mkuranga.

Kati ya vifaa hivyo mifuko 50 ya saruji ni mchango katika ujenzi wa nyumba ya mganga zahanati ya Kijiji cha Koma na mifuko mingine 20 ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kisiju Pwani.

Vullu alielekeza ,Malumalu (tiles)zipelekwe shule ya msingi Kisiju Pwani,katika ujenzi wa vyoo lakini aliomba kipaombele kipewe kwenye vyoo vya wanafunzi wa kike ili kujihifadhi wakati wakiwa katika hedhi .Aidha alisema anahamasisha ujenzi wa nyumba ya mganga na aliwataka wadau wengine waunge mkono jitihada za serikali ,halmashauri ,mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega aliyechangia mifuko 100 ya saruji .

Hata hivyo,Vullu alisema kilichomgusa kuchangia pia ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaelekeza kusimamia maisha na maslahi ya mtanzania .
“Kijiji cha Koma hakina zahanati ,kutokana na suala hilo niliona nguvu za Mbunge ,halmashauri na ndipo Jan 1 ,nikwenda kuona hali ilivyo ,nimeona nitoe fedha za mfukoni mwangu nichangie mifuko ya saruji ujenzi wa nyumba ya mganga .” 

“Vijiji vya huko ni kisiwa ,ukitaka kufika lazima ukitoka ngambo hii hadi nyingine utumie lisaa hadi limoja na zaidi ,wakazi hao wakihitaji huduma zaidi za kiafya inabidi wakimbilie hospital ya wilaya ya Mkuranga ambako ni umbali mrefu “alisema Vullu .

Vullu alisema suala la afya ni muhimu hivyo kuna kila sababu ya kukamilisha ujenzi huo wa zahanati na nyumba ya mganga ili wananchi waondokane na kero yakufuata huduma za afya mbali .

Nae kaimu mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii ,Safina Msemo alishukuru kupata mchango huo.
Safina alisema kwa niaba ya halmashauri, alisema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza nguvu kwenye ujenzi huo .

Kwa upande wake ,mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kisiju Pwani, mwl.Jofrey Mbwale ,alitoa shukrani zake na kusema shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu sita .Alisema kuna walimu nane nyumba zilizopo ni mbili huku alieleza kuna mahitaji ya walimu 20 .
Mwl.Mbwale alieleza mahitaji katika matundu ya vyoo ni matundu 41 yaliyopo ni 20 .

No comments: