Tuesday, February 13, 2018

Tigo Yatoa Zawadi kwa Washindi wa Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 36 wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G. Akitangaza washindi hao wa kwanza 36 waliopatikana katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alibainisha kuwa washindi 13 wanatoka Dar es Salaam, na wengine ni wakaazi wa mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dodoma, Mtwara, Iringa, Mwanza na Arusha. ‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema. 
 Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zaidi ya elfu moja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo kila saa. 
 ‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki. Pia sasa nitaweza kupiga picha za kazi zangu na kuwatumia wateja kwa kasi zaidi kupitia mtandao wa Tigo 4G,’ Said Abdallah Popote ambaye ni fundi wa kupaua nyumba na mkaazi wa Tabata, Dar es Salaam alisema. 
 Advera Salum Abdallah, ambaye ni muuguzi na mkaazi wa Tegeta alisema kuwa simu aliyoshinda itamwezesha mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi kutafiti mambo mbali mbali ya kielimu kupitia mtandao wenye kasi ya juu wa Tigo 4G.
 “Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00# ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Woinde alisema. Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia) akimzawadia   Saidi Abdallah Popote wa Tabata, Dar es Salaam simu aina ya Tecno R6 yenye uwezo wa 4G aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus, huku akishuhudiwa na baadhi ya washindi wengine. Tigo inatoa bonasi ya hadi GB1 ya intaneti kwa wateja wanaonunua bando za data kuanzia TSh 1,000 kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00# pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu za smartphone kila saa.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kati) akimzawadia  Advera Revelian Kyaruzi wa Tegeta, Dar es Salaam simu aina ya Tecno R6 yenye uwezo wa 4G aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus, huku akishuhudiwa na baadhi ya washindi wengine. Tigo inatoa bonasi ya hadi GB1 ya intaneti kwa wateja wanaonunua bando za data kuanzia TSh 1,000 kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00# pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu za smartphone kila saa.

1 comment:

Blogger said...

Ever wanted to get free Google+ Circles?
Did you know you can get them AUTOMATICALLY AND TOTALLY FREE by getting an account on Like 4 Like?