Wednesday, February 7, 2018

POLE POLE AMTAKA MKURUGENZI HALMASHAURI ILALA KUTOA UFAFANUZI MIKOPO WANAYOTOA

Na David John

KATIBU wa Nec Itikadi na uenezi Taifa wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole ameuagiza uongozi wa Chama hicho wilaya chini ya Ubaya Chuma kumuita mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala na wasaidizi wake ili kupata ufafanuzi kuhusu mikopo wanayotoa.

Amesema kuwa pamekuwepo na malalamiko mengi juu ya eneo hilo hivyo lazima viongozi hao wachama Wilaya kuwaita viongozi hao wa Halmashauri ili waje kueleza.

Polepole ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashuri kuu aliyasema hayo katika kongamano la Maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama hicho. Ambapo pamoja na mambo mengine alisema viongozi hao wa Halmashauri waitwe ili waseme fedha hizo wanamkopesha nani.

"Hapa kuna Malalamiko mengi sana kuhusu mikopo hii nani anapewa sasa ndugu Mwenyekiti mwiteni mkurugenz na watu wake muulizeni hizo fedha anapewa nani "amesema Polepole

Nakuongeza kuwa wanachama hawa wa Chama cha Mapinduzi hawapati mikopo,wanamchi.maana hata kwenye maeneo ambako madiwani wa vyama vingine fedha zinakwenda kwa watu wao.

Wakati huohuo Pole amewataka Viongozi na Makada wa Jimbo la Ukonga kushikamana na kufanya kazi kwa uadilifu na upole Kwani kuvurugana kwao ndio kulisabanisha kupeteza jimbo hilo.

Amesema kulikuwa hakuna sababu kwa jimbo hilo kwenda upinzani wakati kijana mwenyewe aliyeshinda ni mtoto wao lakini kama wangesimamisha mtu pendwa jimbo hilo lisingekwenda upinzani.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma aliwataka wanachama hicho kutumia mitandao yao ya kijamii kuzungumzia mambo mazuri kuhusu chama na sikuzungumzia mambo ya hovyo.

" Nasema nitaaza kudili na Maadimini kwasababu hawezi watu wanaandika mambo ya hovyo alafu wanaachwa tu wanatukanwa viongozi lakini bado adimini yuko kimya. "amesema Chuma

Pia amesema amepokea maagizo ya Msemaji wa Chama hicho Taifa nakuhaidi kuwaita viongozi kutoka Halmashauri kama alivyoelekezwa na mkuu wake Taifa.

Kwaupande wake Kada wa Chama hicho ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo kata ya kipawa Geoge Mtambalike alisema ni hatua kubwa kuendelea kukienzi chama hicho kwa vitendo. Aliongeza

No comments: