Wednesday, February 7, 2018

MZEE MWINYI ASHIRIKI KUPANDA MITI NA ROTARY INTERNATIONAL CLUB JANGWANI SEKONDARI

RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa pili kushoto) na Mkewe Esther (wa nne kushoto) pamoja na viongozi wa Rotary Clubs wakimsubiri Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kushiriki nao zoezi la upandaji miti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani Februari 6 2018. Zoezi hilo linaunga mkono kampeni ya mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther Rassin (kulia) wakati District Governor Mteule, Sharmila Bhatt akifanya utambulisho alipowasili kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na District Governor, Kenneth Mugisha wakati Kiongozi wa Rotary Club, Harsh Bhatt akifanya utambulisho alipowasili kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akipungia mkono wananfunzi wa shule ya wasichana ya Jangwani alipowasili shule hapo kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. #RIPEinD9211.Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakimkaribisha Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi alipowasili shuleni hapo kushiriki zoezi la kupanda miti. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitumbuiza wageni wakati wa hafla hiyo
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi kupanda miti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia kwake) District Governor, Bwana Kenneth Mugisha (kulia), Mkewe Esther (wa pili kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211. 
District Governor Kenneth Mugisha akipanda mti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia (kulia kwake) ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa pili kulia) na Mke wa Rais Rassin, Esther (kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitumbuiza wageni wakati wa hafla hiyo. 
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakiwakifuatilia matukio katika hafla hiyo
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) akiagana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti kwenye shule hiyo. Katikati ni District Governor, Kenneth Mugisha. 
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin alipowasili kwenye Wodi ya watoto wenye mahitaji maalum iliyodhaminiwa na Rotary Clubs kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (kulia) akitoa maelezo kwa RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) na District Governor, Kenneth Mugisha. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (kulia) akitoa maelezo kwa RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) na District Governor, Kenneth Mugisha walipotembelea majengo mapya ya hospitali hiyo ambayo Rotary Clubs zimechangia ujenzi wake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi wa Rotary Clubs.
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther Rassin wakiwaangalia watoto wagonjwa wanavyojifunza wakati wakiendelea na matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa ziara yake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs. 
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na mkewe Esther (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Rotary Clubs, walipotembelea walipotembelea majengo mapya ya hospitali hiyo ambayo Rotary Clubs zimechangia ujenzi wake jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni viongozi wa Rotary Clubs na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans (wa nne kushoto).
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin na ujumbe wake wakiondoka baada ya kufanya ziara hospitali ya CCBRT. Anayewasindikiza (wa pili kushoto) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans. 

No comments: