Uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukitembelea bwawa linatumiwa kufundishia wanafunzi ufugaji wa samaki katika Chuo cha Kilimo, Mifugo na Maliasili (Canre), kilichopo Bonyokwa nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Anaye waongoza ni Mkuu wa Chuo hicho, Sylvester Nakara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Myandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Nagamange akionesha kitabu alichotunga cha Wewe ni Bilionea wa Mtaji Sifuri, ambapo aliwaeleza wanafunzi na walimu wa Chuo cha Canre kuwa ili uondokane na umasikini jitahidi kukisoma kitabu hicho chenye mambo mengi muhimu ya kuyafuta hakika muda i mrefu utakuwa tajiri. Kwanza anza na Wazo, Uhusiano na Mawsiliano katika jamii ni muhimu, kusoma vitabu na kuhudhuria mafunzo mbalimbali, usisahau kuwa karibu na vyombo vya habari pamoja na kufanya utafiti kwa yale yote unayotaka kuyafnya ili uwe na uhakika zaidi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Canre, Dk. Aloyce Masanja akizungumza na uongozi wa Mkikita uliomtembelea na kutoa mafunzo kwa wanafunzi na walimu wa chuo hicho kuhusu faida za uwekezaji katika kilimo biashara. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui Steven Kissui, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na Mdau wa Mkikita, Richard
Uongozi wa Mkikita ukiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Canre
Uongozi wa Mkikita ukitembelea maeneo ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo hicho, Nakara akiwaonesha baadhi ya hosteli za chuo hicho
Nakara akitoa maneno ya kuukaribisha uongozi wa Mkikita kutoa mafunzo kwa walimu n wanafunzi wa chuo hicho kuhusu kilimo biashara
Mkurugenzi wa Masoko wa Mkikita, Deo akielezea kwa ufupi kuhusu kazi za Mkikita
Mkurugenzi wa Mkikita anayehusika na utawala na Mashamba, Catherina Edward akitoa maneno ya hamasa kwa wanafunzi kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara badala ya kuendekeza kilimo cha kizamani kisichokuwa na tija
Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema Fredrick akielezea taratibu za mwanachama kujiunga na Mkikita na faida anazoweza kuzipata kwa mfano Mwanafunzi kumiliki shamba litakalosimamiwa na Mkikita na baadaye mapato kuingiziwa kwenye akaunti huku mwanafunzi akiendelea na masomo.
Makamu wa Rais Wanafunzi wa Chuo hicho, Kogea Levi akijitambulisha kwa uongozi wa Mkikita. Kushoto ni Rais wa Wanafunzi wa Chuo hicho, Eliamini Lukwaro na Obedi Sumary ambaye ni Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu wa Canre, Obedi Sumary akijitambulisha
Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza mada zilizokuwa zinatolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange pamoja na viongozi wengine wa mtandao huo
Walimu na watumishi wa Canre wakihudhuria mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Bodi ya Mkikita, Dk Kissui akiwaeleza wanafunzi na waalimu kuwa wakitaka kufanikiwa daima wawe wanaota ndoto kubwa na kuachana na ndoto ndogo zisizo na mafanikio. Pia aliwataka waishi na kufanya mambo kimkakati.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0715264202,068942546 7
No comments:
Post a Comment