Na Said Mwishehe, Glogu ya jamii
WABUNGE
kutoka majimbo mbalimbali nchini kupitia Chama ChaMapinduzi (CCM),
wamewaomba wananchi wa jimbo la Kinondoni jijiniDar es Salaam
kuhakikisha Februari 17, mwaka huu wanamchaguamgombea ubunge wa chama
hicho, Abdallah Mtulia katika uchaguzi
mdogo jimboni humo.
Wamesema
Mtulia ndio chaguo sahihi kwa wananchi wa Kinondoni nakwamba akiwa
mbunge watashirikiana naye katika kufanikishachangamoto za wananchi
zinapata ufumbuzi wake.Pia wameeleza namna ambavyo wabunge wa CCM
wamekuwa wamojabungeni katika kupigania maendeleo ya wananchi tofauti na
wabungewa upinzani ambao kila kitu wao ni kupinga hata liwe jambo
lamaendeleo.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika wanja wa People Kigogo
wilayani Kinondoni jijini, wabunge hao waCCM wamewaomba wananchi
kutofanya makosa kwenye uchaguzi huohuku wakitoa sababu mbalimbali za
kwanini Mtulia anastahili kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mgeni
rasmi kwenye kampeni hizo ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein
Bashe (CCM) amewaomba wananchikumchagua Mtulia kwani ndio mgombea
sahihi na wanaamini akiwambunge watashirikiana naye kutatua kero za
wananchi.
"Nimekuja
kuzungumza na ninyi kuwaomba tarehe 17,siku yaJumamosi wote mkamchague
Mtulia, lakini si tu kumchagua lazimatuseme kwanini mumchague
Mtulia.Ndio mgombea mwenye sifa zoteza kuwa mbunge wa Kinondoni,"amesema
Bashe.
Pia
amesema kwenye kampeni hizo wapo wanaotoa hoja kuwa Serikali ya CCM
haitaki mfumo wa vyama vingi, ambapo amefafanua hoja hiyo haina maana
yoyote kwani mwaka 1992 licha ya watanzania wengi kutaka mfumo wa chama
kimoja uendelee lakini uamuzi ulitolewa wa kuingia mfumo vyama vingi.
"Mwaka
1992, watanzania walipata fursa ya kuchagua tuingie kwenye mfumo wa
vyama vingi au laa.Waliotaka vyama vingi walikuwa asilimia 20 na
waliosema chama kimoja kiendelee walikuwa asilimia 80."Mwaka 1995
tukafanya uchaguzi wa vyama vingi na CCM ikashinda, hivyo CCM hatuna
hofu na mfumo wa vyama vingi na ndio maana tumeendelea kushinda katika
kila chaguzi.
"Pia
wapo wanaotoa hoja CCM hakuna demokrasia hili nalo halina ukweli.CCM
demokrasia ipo tena ya kutosha.Ndani ya CCM tunaweza kutofautiana
kimtazamo, tunaweza kutofautiana kwa hoja na wakati mwingine tukashikana
mashati lakini ukweli utabaki tunafanya hayo yote kwasababu ya
demokrasia tuliyonayo,"amesema Bashe.
Kuhusu
hoja uchaguzi ni gharama, Bashe amesema wanaona ni gharama wanayo fursa
ya kupeleka muswada wa sheria bungeni ili kubadilisha sheria ambayo
itaelekeza hakuna uchaguzi mdogo hata mbunge anapoamua kuondoka chama
kimoja na kujiunga na chama kingine.Pia njia nyingine ni kubadilishwa
kwa sheria ili kurudi kwenye mfumowa chama kimoja ambao hautakuwa na
gharama.
"Kuna
hoja nyingine hazina maana mbunge akitoka upinzani kwendaCCM wanasema
kanunuliwa ila akitoka CCM kwenda upinzani huyohajanunuliwa.Hii hoja
haina mantiki yoyote.
Bashe
amesema Mtulia ameamua kujiunga CCM ili aweze kuleta maendeleo ya
wananchi kwani alikokuwa hakuko salama."Mtulia mwaka 2015 alikuwa kwenye
gari ya Ukawa na sasaameamua kuwa kwenye gari la CCM.Tatizo liko wapi
hasa kwakuzingatia kule alikokuwa hakuko salama.CUF imegawanyika vipande
viwili kwani Katibu Mkuu wao, Maalim Seif Sharif Hamad anafanya
kazi
kivyake na Mwenyekiti Lipumba naye yupo kivyake."Mtulia alikuwa anapata
posho bungeni, analipwa mshahara lakini ameamua kujiuzulu kutokana na
hali iliyopo kwenye chama chake kwani hakuwa anapata muda wa kutosha
kushughulikia changamoto za jimbo lake.Akaona ni bora ajiuzulu kule na
kisha aje huku,"amesema Bashe.
Mke
wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum
Mkoa wa Lindi, Salma Kikwete amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua
Mtulia ili washirikiane naye kutatua changamoto za wananchi wa Tanzania
wakiwamo wa Kinondoni.Amesema Rais ,Dk. John Magufuli anafanya kazi
nzuri ya kuleta maendeleo ya wananchi ,hivyo ni vema Kinondoni
wakamchagua
Mtulia
ili awe sehemu ya kiunganishi kati ya Rais na wananchi."Kazi iliyopo
mbele yenu ni kumchagua Mtulia ili awe mbunge wa Kinondoni. Wabunge na
viongozi wa ngazi mbalimbali ndio maana wapo hapa kumuombea kura Mtulia
awe mbunge kwani wanaamini atashirikiana nanyi katika kupigania
mamboyanayowahusu,"amesisitiza Mama Salma.
Kwa
upande wake Mbunge Geita Vijijini, Joseph Kasheku mbali ya kumuombea
kura Mtulia ametumia nafasi hiyo kuwaeleza baadhi ya viongozi wa Chadema
kuwa hawana tofauti na watu matapeli.Amemtolea mfano Frederick Sumaye
ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 lakini hakuna hata siku moja
ambayo amekwenda kuhutubia wananchi wa Kigogo lakini baada ya kuona kuna
uchaguzi wa ubunge ndio anakwenda.
"Sumaye
amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 lakini hajawahi kufika kuhutubia
wananchi na leo maisha yamempiga ndio anakuja kwenu.Wananchi msihangaike
ikifika siku ya uchaguzi Februari 17
nendeni
mkamchague Mtulia aje bungeni."Tena akifika bungeni nitamwambia
akamuombe Spika wa Bungetuwe tunakaa karibu ili niwe namuelekeza ...
mimi ni darasa la saba lakini mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi
hayana nafasi,"amesema.
Pia
amesema upinzani wanazungunzia namna ambavyo viongozi wa CCM wanapiga
magoti wakati wa kumuombea kura Mtulia na kueleza hiyo ni ishara ya
heshima na ndio sifa ya wanaCCM ya kuheshimu wananchi.Wakati huo huo,
Mbunge wa Mtela, Livingston Lusinde naye ameendelea kumuombea kura
Mtulia huku akitumia nafasi hiyokuwapiga vijembe wapinzani kutokana na
hoja mbalimbali wanazozitoa kwenye kampeni hizo.
CCM
kwenye kampeni hizo wamekuwa wakitumia wabunge wake mbalimbali pamoja
na viongozi ambao wamekuwa wakimuombea kura Mtulia na kwa kampeni za
leo zilizofanyika Kigogo wabunge zaidi ya10 wamemuombea kura mgombea
wao.
No comments:
Post a Comment