Na Said Mwishehe
KWA heshima na taadhima, naomba nitumie nafasi hii kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Natoa
salamu zangu kwenu nikitambua kuwa pamoja na shughuli nyingine za
ujenzi wa nchi yetu , pia mpo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo
hilo.Sababu za kufanyika za uchaguzi huo unatokana na uamuzi wa
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF)
Maulid Mtulia kuamua kujiuzulu ubunge.Baada ya kujiuzulu akaondoka CUF
na kujiunga CCM.
Sioni
umuhimu wa kurudia sababu ambazo amezitoa Mtulia wakati anatangaza
kujiondoa CUF.Hata hivyo moja ya sababu amedai alipokuwa CUF alijikuta
akiwa kwenye wakati mgumu kutokana na mpasuko uliopo.Tunafahamu
ndani ya CUF hakuko sawa kutokana na tofauti ya misimamo na mitazamo
baina ya vingozi wa juu wa chama hicho.Hivyo Mtulia akaona bora ajiweke
kando.Ndio sababu ambayo ameitoa.
Pia
akasema
juhudi za Rais ,Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo zimemfanya aone
haja ya kuunga mkono kwa kujiunga na CCM.Najua kila mtu anayo nafasi ya
kuchambua na kupima anachosema Mtulia.Kwa sasa Mtulia anagombea tena
ubunge wa Kinondoni kwa tiketi yaCCM.Kampeni zinaendelea Kinondoni na
Mtulia ni miongoni mwa wanaomba kura kwa wananchi.
Katika uchaguzi huo ushindani upo kati ya Mtulia na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Salimu Mwalimu.Ni
ushindani haswa na kila chama kilipozindua kampeni rasmi walitoa tambo
nyingi.Tunasubiri mwisho wa tambo hizo utakuaje.
Kila
mmoja anaamini ataibuka na ushindi.Chadema wanaamini Kinondoni ni ya
Salumu Mwalimu na hivyo hivyo CCM nao wanaamini Kinondoni ni ya
Mtulia.Sawa
yupo mgombea wa TLP ,Dk.Godfrey Malisa ambaye naye anawania jimbo
hilo.Najua wapiga kura ndio wenye kuamua nani awe mbunge wao baada ya
kila mmoja kupita na kutoa sera za chama chake kuhusu nini watafanya
kwenye jimbo hilo.
Pamoja na kwamba wananchi wa Kinondoni ndio wa kuamua bado ukweli uko pale pale wenye ushindani zaidi upo kwa Mtulia na Salum
Mwalimu.Nikiri na kusisitiza wananchi wa Kinondoni wao ndio waaamuzi wa
mwisho.Yangu macho tu na kueleza ninachoona kwa sasa.
Nikumbushe
kidogo tu.Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,Mtulia aligombea Kinondoni na
akashinda.Alishinda kwa sababu wananchi waliamini ni mtu sahihi
kwao.Mtulia alipambana na Idd Azan (CCM) lakini akambwaga kwa wingi wa
kura.Salum Mwalimu wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliamua kwenda
kugombea jimbo la Kikwajuni visiwani Zanzibar.Hakushinda uchaguzi huo.
Hivyo
tukiangalia uchaguzi mkuu uliopita utaona Mtulia alipewa imani na
wananchi wa Kinondoni.Mwalimu hakuwa ameshinda kwa kule Kikwajuni.Sina
maana atashindwa na uchaguzi huu maana mazingira ni tofauti na uchaguzi
mkuu, lolote linaweza kutokea.
Hata
hivyo kwa
Salum Mwalimu yeye kugombea jimbo la Kinondoni, ndio mara yake ya
kwanza.Sote tunafahamu kura ni siri ya mpiga kura hivyo anaweza kushinda
Mwalimu au Mtulia ama Dk.Malisa.Kwa yoyote atakayeshinda hakuna dhambi,
kikubwa inategemea wanachanga vipi karata zao katika kipindi hiki cha
kampeni.Yangu macho.Wananchi wa Kinondoni ndio wataamua nani awe mbunge
wao.Kupitia kampeni zinazoendelea watawafahamu wagombea wao vizuri na
vyama vyao.
Sijui
nikoje? Yaani kila nikiwaza uchaguzi huo naona ni vema nikatoa ushauri
wangu kwa wananchi wa Kinondoni.Naamini ushauri wangu mtaukubali..Ila
hata mkiukataa hakuna tatizo lakini nimeshauri tayari.Ni hivi naomba
muwasikilize wagombea wote tena kwa umakini mkubwa.Wasikilizeni kila
wanachosema na kila wanachowaaahidi.Mwisho mtakuwa na nafasi ya kuamua
nani atakuwa sahihi kwenu.
Huu
si wakati wa kuchagua mbunge kama vile mpo kwenye ushindani wa Simba na
Yanga.Uchaguzi mdogo unamaana kubwa licha ya kuitwa ni uchaguzi
mdogo.Ni uchaguzi unaotokana na jimbo
kuwa
wazi baada ya aliyekuwepo kuamua kujiuzulu kwa sababu ambazo amekuwa
akizielezea.Hivyo kwa mujibu wa Katiba yetu lazima uchaguzi ufanyike.
Tayari
Serikali iko madarakani na kila mwananchi anajua hilo.Hivyo kinachobaki
ni kupata mbunge ambaye atakuwa mwakilishi wawananchi
bungeni.Wanachagua mbunge atakayechukua changamoto za wananchi na kisha
kuzipeleka kwenye vyombo vya mamlaka zipatiwe ufumbuzi wake.
Mnachagua
mbunge ambaye atapinga kwa hoja na si kupinga hoja kwa vioja na
vituko.Ni jukumu la wananchi wa Kinondoni kuamua kati ya Salumu
Mwalim,Maulid Mtulia na Dk.Malisa nani mnaona mkimpa nafasi itakuwa
rahisi kumtuma.
Wapo
wanaosema fedha nyingi zinatumika kwenye uchaguzi huomdogo.Fedha ambazo
zingeweza kutumika kwenye mambo mengine yakimaendelea.Wanaweza kuwa na
hoja lakini ifahamike demokrasia nigharama na haziepukiki.Zipo tu.Kama
una bisha shauri yako.Ndio maana kote ambako wabunge walitangaza kuachia
majimbo uchaguzi umefanyika tena.Si jambo jipya hata huko nyuma
kumeshafanyika chaguzi ndogo mara nyingi tu.Unabisha nini?Huenda
umesahau acha nikukumbushe uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga baada ya
Rostam Aziz kuamua kujiuzulu.Ni moja tu ya mfano kati ya mingi.Fedha
zilitumika kama ambavyo zinatumika sasa.
Hata
ikitokea mbunge aliyepo amefariki lazima Tume ya Taifa
Uchaguzi(NEC)itangaze kufanyika kwa uchaguzi mdogo.Huo ndio utaratibu
iwe ni gharama kubwa au ndogo.Kwa wananchi wa
Kinondoni kikubwa kwenu ni kuchekeka na kuwapima wagombea waliopo mbele
yenu na kisha kupata mtu sahihi ambaye mtashirikisha naye kutatua kero
zenu.
Tunafahamu uchaguzi huo wa Kinondoni kwa
vyama vya upinzani ni kipimo cha wao kama bado wanaendelea kuaminika kwa
wananchi au la.Na kwa CCM nao ni uchaguzi ambao wanautazama kwa jicho
la aina yake.Ni uchaguzi ambao unatoa picha ya namna ambavyo wananchi
wanawaamini kwa kiwango gani.
Kimsingi uchaguzi
wa Kinondoni ni uchaguzi mdogo kama ambavyo tunaelezwa lakini umebeba
sura ya kitaifa kutokana na mazingira yaliyopo.Nimalize tu kura
zitakazopigwa siku ya uchaguzi zitatoa majibu ya nani anatakiwa na
wananchi wa Kinondoni.Yangu macho maana huku namuona Mtulia na kule
namuona Mwalimu.
TUWASILIANE
0713833822
No comments:
Post a Comment