Friday, February 23, 2018

MABULA ASHANGAZWA UTATA KATIKA UMILIKI WA HATI ZA ARDHI

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akizungumza na watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya ya musoma mkoa wa Mara.
Baadhi ya watumishi wa kanda wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula wakati wa ziara yake mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vicent Anney Naano akizungumza wakati wa ziara ya naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mkoani mara.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoa wa Mara.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akimkabidhi majalada ya ardhi afisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Hamida Marenda kwa ajili ya uchunguzi.



Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mhe. Angelina Mabula ameshangazwa na uwepo wa majalada ya ardhi katika halmashauri za Butiama na Musoma ambayo wamiliki wake hawafahamiki na majalada hayo kujulikana kama ‘’ndugu mhusika’’.

Akiwa katika ziara yake ya siku tatu ya kushughulikia migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ulipaji kodi ya ardhi mkoani Mara mhe. Mabula alisema majalada hayo yamekuwa na matatizo ya viwango vya kulipa kodi kwa kuwa yanaonekana kuwa deni huku mmiliki akitaka kumilikishwa upya kwa gharama ndogo.

Kufuatia mkanganyiko huo, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliyakabidhi majalada yenye utata kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama suala hilo limefanyika kimakosa ama ni kwa makusudi.‘’Mtu anamilikishwa leo kwa pesa ndogo sana halafu za huko nyuma zinapotea hapa kuna mchezo unafanyika kupunguza mapato ya serikali’’ alisema Mabula.

Aidha, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ametaka majalada ya ardhi kuingizwa katika mfumo kwa kila robo ya mwaka ili iwe rahisi kufuatilia waliolipa kodi ya ardhi na wale wasiolipa.Kwa mujibu wa Mabula tatizo baadhi ya watumishi hawana nia thabiti ya kutumia mfumo wa kukusanya maduhuli ya serikali ndiyo maana utekelezaji wa maagizo yanayotolewa unashindwa kufanikiwa.

Awali mkuu wa wilaya ya Musoma Dk. Vicent Anney Naano alimueleza naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuwa wilaya yake ina changamoto kubwa ya watumishi wa ardhi, ukosefu wa ramani za vijiji, kutoendelezwa kwa baadhi ya viwanja na wananchi wengi kutokuwa na fedha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao.

No comments: