Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.
Amesema
kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao
wengine wageuza Chama ni mali yao na kutoamaamuzi ambayo si shirikishi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Katambi
amesema kuwa tanguameondoka Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana
na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa kimya muda mrefulakini
ameona ni vema akasema mambo kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.
Kuhusu
vyama vya siasa kuyumba, Katambi amesema zipo sababuambazo zimekuwa
zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara namatokeo yake kubaki
kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa naSerikali hata liwe lenye
maslahi kwa nchi.
"Upinzani
umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kilachama ni cha
mtu.vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana yataasisi ni kwamba
sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe"Kama mtu anadharau katiba na
misingi iliyowekwa basi huo niudikteta. Wapinzani kabla ya kukimbilia
kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza kujenga taasisi, kama
wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao wanapate uhalali wa kudai
Katiba,"amesema.
Amesema
sababu nyingine vyama vya upinzani vimekosa uamuzi shirikishi."Chadema
ambayo inajieleza ni chama cha upinzani chenye nguvukimeshindwa kuwa na
utaratibu wa kuwa na maamuzi shirikishi nahata yanayoamriwa ni maamuzi
ya mtu.Na pia kuna ukiukwaji wauteuzi wa nafasi ikiwamo za ubunge viti
maalumu ambao umetawaliwana rushwa na kupeana nafasi kirafiki.
"Tatizo
la upinzani hakuna kuheshimiana na ukosefu wa maadili yaviongozi. Kama
Taifa lazima liwe na viongozi wanaozingatia maadili,kwa mfano leo hii
Ukawa wakichukua nchi nani anaweza kuwa WaziriMkuu,"amesema.
Kada
huyo wa CCM, amesema kuwa vyama vya upinzani adui yaomkubwa ni CCM
lakini wameshindwa kuwa na uwazi kwenye mali zaokwani hata Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),akikagua ni lazima atapata hati
zenye shaka kwani fedha za ruzukuzinatumika vibaya.
"Wanaosema
nimenunuliwa wanajidanganya kwani wakati anakwendachadema wamemnunua
kwa shilingi ngapi. Kuna wabunge zaidi ya 15wataondoka Chadema na kuna
wajumbe wapo ndani ya chama hicholakini tayari wameshaondoka ila
wanaingia kwenye vikao ili kutimizawajibu tu," amesema Katambi.
Amesema
kwa sasa vyama vya upinzani wamekosa ajenda na waliopo huko wanakwenda
tu bora liende na wengine wanajua wakitoka hawataajirika."Kukosea
ajenda chadema walikuwa wanasema wanapambana naufisadi na hata slaa
aligeukwa kwa sababu ya masilahi ya watu binafsi.Chadema ya Dk. Slaa
kila mtu anaifahamu ilifika wakati akapelekwaMarekani kwa ajili ya
kuandaliwa ili aje kuwa Rais lakini baadaye wakaanza kumtuhumu kwa
usaliti," amesema
Kutokana
na hali hiyo amesema kuwa sasa umefika mwisho wa Umojawa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kwani malengo ya Chademayametimia kwa kuua nguvu ya
kila chama ili wabaki wao katikaupinzani.
No comments:
Post a Comment