Mchungaji wa Mji Mtakatifu na kazi nyingine za Palestina na
Jordan Theophilus III, kwa niaba ya wachungaji na viongozi
wote wa Makanisa ya Jerusalemu (Makanisa ya Kigiriki,
Kikatoliki na Kiarmenia),katika hatua ambayo haijawahi
kutokea, Jumapili iliyopita ametangaza kulifunga Kanisa hilo
la Ufufuo lililopo Jerusalemu ya kale hadi itakapotolewa
taarifa nyingine,ikiwa ni kutokukubaliana na kupinga kwao
na sera za utawala wa kivamizi wa Israeli dhidi ya Makanisa
na kuyataka yalipe kodi.
Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika katika kiwanja cha Kanisa hilo la
Ufufuo,ikiwa ni kupinga vitendo vya utawala wa kivamizi
dhidi ya makanisa hayo. Kwani utawala huo hivi karibuni
umeyataka Makanisa hayo ya Jerusalemu yalipe kodi ya mali
ijulikanayo kama"Arnona",yenye thamani ya shekel milioni
kila mwaka, huku ukiingilia mali za Kanisa la Orthodox la
Kirumi kwa lengo hilohilo.
Nao Viongozi wa Makanisa ya Jerusalemu katika mkutano
wa waandishi wa habari, wametoa tamko wakisisitiza ya
kwamba,”Kuyatoza kodi Makanisa mjini Jerusalemu ni
ukiukwaji wa mikataba yote iliyopo na wajibu wa kimataifa
unaodhamini haki za Makanisa na mambo yake maalumu."
Tamko hilo limesisitiza kuwa, hatua hiyo ni "jaribio la
kudhoofisha uwepo wa Kikristo katika jiji hilo," Huku
likionya kuupitisha mpango wa kamati ya wizara iliyo chini
ya utawala wa kivamizi wa Israeli wa kutoza kodi kwa
Makanisa mjini Jerusalemu,ambao unafanyika kupitia
kuchukua kwa nguvu ardhi ya Makanisa hayo yaliyo mjini
hapo.
Serikali ya Palestina imeizingatia hatua ya utawala wa
kivamizi kutoza kodi nyumba za ibada yakiwemo makanisa,
kuwa ni uadui mpya dhidi ya wananchi na maeneo yake
matakatifu, jambo lililopelekea kufungwa kwa kanisa la
Ufufuo lililopo katika mji mkuu unaokaliwa kimabavu. Huku
ukiuchukulia uadui huo mpya kuwa unalenga mji wa
Jerusalemu na taifa letu lote la kiarabu la kipalestina pia
unagusa maeneo yake matakatifu, huku likionya juu ya
madhara makubwa yanayoweza kunyakua ardhi za makanisa.
Serikali imeomba kuingilia kati kwa haraka kwa jumuiya ya
kimataifa ili kusitisha vitendo hivyo vya Israeli, ambavyo
vinahesabiwa kuwa ni mashambulizi mabaya ya
mikataba,makubaliano na desturi zote za kimataifa,
vinavyodhamini uwepo wa uhuru wa kuabudu na kuheshimu
utakatifu wa sehemu za kidini,katika hali yoyote na popote.
Serikali pia imetoa wito maalumu kwa ulimwengu wa kikristo
na kiislamu, wa kuchukua hatua stahiki kwa ngazi zote ili
kuzuia vitendo vya kivamizi, vinavyolenga kwa kiwango sawa
sehemu takatifu za kikristo na kiislamu.
Kwa upande mwingine, mwanachama wa Kamati Tendaji ya
Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina Mheshimiwa ”Hanan
Ashrawi” katika tamko lake rasmi alilolitoa, amelaani
mashambulizi mabaya ya Israeli dhidi ya makanisa na
sehemu takatifu za kikristo mjini Jerusalemu, ukiwemo
uamuzi wa hivi karibuni wa Manispaa ya kivamizi kutaka
kodi ijulikanayo kama"Arnona" kutoka katika mali za Kanisa
lililopo Mji Mkuu unaokaliwa kimabavu.
Ashrawi amesema kuwa, “Makanisa ya Kikristo yapo katika
ardhi hii muda mrefu kabla ya kuanzishwa kwa Israeli na
kwamba utambulisho wa Palestina unajumuisha urithi wa
kale zaidi wa Kikristo unaoendelea kuwepo, ukiwa ni
sehemu ya uwepo wa Palestina wa asili katika ardhi hii.
Dola ya Israeli kwa hatua hizi za hatari, inakiuka vibaya
hali iliyopo ambayo ndio msingi wa hali ya makanisa ya
kikristo nchini Palestinakwa karne nyingi”.
Ashrawi ameongeza kusema kuwa, sheria za Israeli za hivi
karibuni zinakuja katika mazingira ya kuimarisha mwelekeo
wa dola ya kivamizi, wenye sera za uhamisho wa nguvu na
usafisho wa kikabila kwa lengo la kufuta uwepo wa Palestina
na kuitenga Jerusalemu na eneo lake. Pia kwa makusudi na
njia ya moja kwa moja huenezwa makanisa, akaunti na mali
zake, ili kuimarisha udhibiti wa Israeli wa Mji Mtakatifu na
kuongeza nguvu uwepo wa wayahudi wenye itikadi kali, kwa
kuwaondosha wakazi wa asili wa mji huo.
Ameongeza kusema kuwa,hakika Israeli inafanya hasa
uhamisho na kushambulia kwingine, kama ulivyo uvamizi
wake wa kijeshi usio wa kisheria unakiuka moja kwa moja
uhuru wa kuabudu kwa dini zote. Huku ikifanya ubaguzi
mbaya kupitia sera zake zilizo rasmi dhidi ya wapalestina
wakristo na waislamu kwa namna iliyo sawa.
Akasisitiza ya kwamba sera za Israeli, hatua zake na sheria
zake,inaaibisha madai yake kuwa inalinda uhuru wa kuabudu
kwa dini zote, tokea uvamizi wake Ukingo wa Magharibi na
Ukanda wa Gaza mwaka 1967, Israeli imewazuia kwa namna
iliyoratibiwa wananchi wa Palestina wakiwemo wakristo na
waislamu kufika katika maeneo matakatifu ya ibada yaliyopo
mjini Jerusalemu, kama walivyowazuia wakazi wa
Jerusalemu kupata huduma muhimu zikiwemo afya na elimu.
Katika mtiririko huohuo, Mamlaka ya Hashimiya ya Jordan
imelaani hatua hiyo ya Utawala wa Kivamizi wa Israeli dhidi
ya Makanisa ya Jerusalemu na mali zake, kiuzingatia
Utawala huo kuwa unakiuka sheria za kimataifa,huku
ikiutaka "Kuachana na hatua yake hiyo mara moja".
Hayo ameyasema Waziri wa nchi katika Mambo ya habari
ambae pia ni Msemaji Mkuu wa serikali Mheshimiwa
Muhammad Al Muumaniy,ambapo amesisitiza
kutokukubaliana kabisa kwa Mamlaka hiyo na hatua hiyo ya
Israeli iliyoratibiwa, katika kubadilisha hali ya kihistoria na
kisheria iliyopo katika maeneo matakatifu mjini Jerusalemu
ya Mashariki, zikiwemo mali na wakfu za kiislamu na
kikristo.
Al Muumaniy amesisitiza kwamba,"Hakika hatua hizi
zinapuuza sheria za kimataifa, sheria za kibinadamu za
kimataifa na mpango wa hali ya kihistoria uliopo tokea
miaka mingi",huku akiashiria kwamba "makanisa siku zote
yamesamehewa kulipa kodi kwa tawala za kiraia zilizopo
mjini". Ameitaka Israeli "kuacha haraka maazimio yake
iliyoyapitisha dhidi ya Makanisa na kuheshimu wajibu wake
kwa mujibu wa sheria za kimataifa,kama ndio nguvu
inayoweka uvamizi katika Jerusalemu ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment