Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kushoto akiwakabidhi wafanyabiashara soko kuu TV na king'amuzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyomshinda mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) miaka 10 toka ahahidi
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ,katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wakiwa na wafanyabiashara baada ya kutekeleza ahadi iliyomshinda mbunge Msigwa
Na MatukiodaimaBlog
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimetekeleza ahadi ya TV iliyoahidiwa wakati wa kampeni za ubunge mwaka 2015 na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika soko kuu la Manispaa ya Iringa .
Akizungumza leo mara baada ya kukabidhi TV hiyo na king'amuzi chake kwa uongozi wa soko kuu mjini Iringa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa CCM imelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya TV nchi 58 baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kuomba kusaidiwa TV hiyo kwa ajili ya kufuatilia habari mbali mbali zinazojiri nchini wakiwa katika sokoni hapo .
Alisema pamoja na kuwanunulia TV hiyo aina ya Sumsung wamepata kuwanunulia king'amuzi pamoja na kuwalipia malipo ya mwezi mmoja kuwa lengo la CCM kufanya hivyo ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbali mbali za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao .
" CCM tumeendelea kutekeleza ahadi mbali mbali ila kama mtakumbuka kata ya Kihesa kulikuwa na jengo ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka 10 ila baada ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kihesa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri aliahidi na tayari ametekeleza hivyo CCM tukiahidi tunatekeleza wenzetu wakiahidi wanatelekeza ahadi zao "
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Magufuli aliwaagiza viongozi wa CCM kwenda kutatua kero za wananchi na ndivyo ambavyo CCM Iringa mjini imekuwa ikifanya hasa ukizingatia kuwa chama kinachotawala ni CCM hivyo lazima CCM kutatua kero za wananchi bila kujali zilitolewa na upinzani ama CCM .
" Hatupendi kuona wananchi wanasikitika ama wanapoteza haki zao hivyo tutawasikiliza na kutatua kero zao wenzetu wanaahidi bila kutekeleza ila sisi kama CCM tutahakikisha ilani yetu inatekelezwa kwa nguvu zote na tutakwenda tena kuwasikiliza wanahitaji nini "
Katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga alisema kuwa kuwa pamoja na CCM kutekeleza ahadi ya mbunge Msigwa wa Chadema ila imeendelea kusaidia jamii katika shughuli za maendeleo kama kutoa bati 300 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na kutoa elimu kwa wanawake juu ya ujasiliamali .
Alisema kuwa kutoka na wapinzani kufanya kazi ya kwenye mitandao ya kutukana na kubeza CCM ila wao CCM kazi yao ni kuwakomboa wananchi na kuona wanatatuliwa kero walizo nazo na kudai kuwa kwa kazi zinazofanywa na CCM Iringa mjini ndizo zinapelekea madiwani zaidi ya Chadema kujiuzulu na kujiunga na CCM .
" Hadi hivi sasa CCM toka madiwani wa kata watatu sasa ina madiwani 9 waliohamia CCM hivyo ndio maana tunasema madiwani waliobaki nje ya CCM wajiunge na CCM timu ya maendeleo maana shabaha kubwa ni kuwatumikia wananchi "
Katibu huyo wa CCM Iringa mjini alisema kumekuwepo na maneno mengi yasiyo ya kweli juu ya CCM kununua madiwani wa Chadema na kuwa suala hilo halipo kwani CCM haina pesa za kununua diwani ina pesa za kuwaletea wananchi maendeleo .
Mwenyekiti wa soko kuu la Iringa Sturmi Fussy akishukuru kwa msaada huo alisema kuwa TV hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wafanyabiashara sokoni hapo kwani itawapunguzia muda wa kutoka katika eneo lao la kazi kwenda kutazama TV nje ya soko hilo hata hivyo aliomba CCM kusaidia daladala kufika eneo hilo la soko ili kuongeza wateja zaidi katika soko hilo
No comments:
Post a Comment