Friday, February 9, 2018

BoT YAWAASA WAANDISHI KUTOA UCHAMBUZI WA KINA TAARIFA ZA FEDHA ZA MABENKI

Kaimu Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Mtwara, Bi. Leticia Rweyemamu, akitoa hotuba ya kufunga semina ya sikju tano ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha, kwenye makao makuu ya tawi hilo Mkoani Mtwara leo Ijumaa Februari 9, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara

SEMINA ya siku tano ya waandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania, Idara ya Uhussiano na Itifaki, imemalizika leo Februari 5, 2018 mkoani Mtwara.

Katika simian hiyo iliyofunguliwa mwanzoni mwa wiki na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC), Bw. Julian Raphael Banzi, waandishi hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya mfumo mpya wa kuandaa Sera ya Fedha, (Financial Monetary Policy), mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia, mifuko ya dhamana kwa wajasiriamali na dhamana za serikali. 

Mambo mengine ambayo waandishi hao kutoka vyombo mbalimbali vikiwemo, Redio, Luninga, Magazeti na Blogs ni kanuni mpya za usimamizi wa bureaux de change, usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha na dhamana kwa mikopo ya nyumba (Mortgage Finance). 

Waandishi hao pia wamepata wasaa wa kujifunza nafasi ya matawi ya BoT katika utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo, fidia za interoperability katika kukuza huduma rasmi za fedha ili kujua kuna usalama gani wa fedha za wateja wanaotumia mifumo ya kufanya miamala ya kampuni za simu. 

Lakini pia wamejifunza kuhusu nafasi ya dodi ya ya amana katika ufilisi na kwa nini ulipaji fidia kwa wateja wa benki zilizofilisiwa unachukua muda mrefu, mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa Sera ya Fedha Safi (Clean Money Policy), mafanikio na changamoto za dawati la kutatua malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha. 

Aidha waandishi hao pia walipata fursa ya kutembelea miradi ya kiuchumi inayotekelezwa na serikali na taasisi binafsi ya uchimbaji na uc hakataji wa gesi, huko Mnazi-Bay na Madimba. 

Akifunga semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa BoT tawi la BoT, Mkoani Mtwara, Bi. Leticia Rweyemamu, amewataka waandishi hao kutumia elimu waliyoipata ili kuhabarisha umma kwa usahihi kuhusu kazi za Benki Kuu, na kutumia faida waliyopata ya kukutana na wataalamu mbalimbali wa BoT ili wawatumie kupata ufafanuzi wa habari mbalimbali za kiuchumi ili kuandaa habari timilifu. 

“Nimejifunza kutoka kwenu kwamba ubora wa habari unategemea idadi ya watoa taarifa katika habari hiyo na ninatoa rai kuwa watumieni wataalamu hao ipasavyo ili kuzifanya taarifa zenu kwa wananchi ziwe bora zaidi.” Alisema Bi. Rweyemamu 

Aitoa wito kwa waandishi hao kutumia utaalamu kuelimisha umma kutumia huduma rasmi za kibenki ili kutunza fedha na kufanya miamala kwani ni muhimu kwa sababu licha ya kuhakikisha usalama wa fedha za mtyumiaji wa huduma hizo kuna uwezekano mkubwa wa kujikinga na upotevu wa fedha unaoweza kutokea kwa sababu mbalimbalin ikiwemo wizi. 

“Pia toeni uchambuzi wa kina kuhusu taarifa za fedha, (Financial Statements), za mabenki na taasisi za fedha ili kuwawezesha wananchi waliokuwa na amana au wangependa kuwekeza amana zao kuwa na taarifa sahihi kuhusu hali ya taasisi hizo ili kufanya maamuzi sahihi. 

“Haitoshi kuandika kuwa benki fulani imepata faida kiasi Fulani au hasara kiasi Fulani tu, ni vema wananchi wakapata taarifa mbalimbali zinazohusu ukwasi wa taasisi husimka, ikiwemo mali, madeni pamoja na mipango mbalimbali ya taasisi hizo za kifedha.” Alifafanua. 

Bi. Rweyemamu, amewahamasisha waandishi hao kutumia nafasi ya BoT kuhabarisha namna inavyoandaa na kutekeleza sera ya fedha ili kuhabarisha umma mwenendo wa uchumi na sekta ya fedha nchini ili hatimaye wafanye maamuzi sahihi ya kuhusu uwekezaji hapa nchini. 

Alivitaka vyombo vya habari kutumia nafasi kubwa katika kutoa taarifa zinazochangia maendeleo ya uchumi wa viwanda na kupunguza fursa kubwa inayotolewa kwa taarifa za kuburudisha tu, kwani kwa kufanya hivyo vyombo vya bhabari vitaisaidia serikali kuelezea mipango yake ya kueldekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. 

“Kama alivyoeleza Naibu Gavana wakati akifungua semina hii, Benki Kuu inatambua mchango wa vyombo vya ahabari vyote ikiwemo redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii katika kutangaza habari za benki hiyo kwa manufaa ya umma.” Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina alisema BoT itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kwani kwa kufanya hivyo kunajenga uwezo wa waandishi kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali na kuziandika kwa usahihi. 

“Nimefarijika sana kuwa pamekuwepo na uelewa mkubwa wa waandishi hawa kuhusu utekelezaji na majukumu ya Benki Kuu.” Alisema 
Kaimu Meneja wa Idara ya Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina, akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa semina hiyo.
Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo Februari 9, 2018.
Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT, akiwasilisha mada kuhusu Government securities (Government Date Securities) , mwishoni mwa semina hiyo leo Februari 9, 2018.
Baadhi ya washiriki wakifurahia hotuba ya mgeni rasmi.
Bw. Abdueli Elinaza akitoa hotuba kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo.
Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano, akitambulishwa kwa wana semina kabla ya kuwasilisha mada ya mafanikio na changamoto za dawati hilo.
Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Bw.Ganga Ben Mlipano, akiwasilisha mada kuhusu mafanikio na changamoto za dawati la kutatua malalamiko ya wateja wa benki na taasisi za fedha.
Bw. Ganga akibadilishana maewazo na Bi.Vicky Msina, kabla ya kuwasilisha mada yake.
Mgeni rasmi, B. Leticia Rweyemamu, (kulia), akiongozana na Bibi.Leah Mzundu, Meneja Idara ya Uendeshaji Tawila BoT Mtwara, wakati akiwasili ukumbini kufunga semina.
Kutoka kushoto, Bi. Vicky Msina, Bi. Leticia Rweyemamu na Dkt. Suleiman Missango.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji na wana semina mwishonin mwa semina hiyo.

No comments: