Tuesday, February 27, 2018

MNEC SALIM ASAS ATOA MSAADA WA MILIONI TANO KWA JUMUIYA YA WAZAZI KILOLO




Na Fredy Mgunda,Kilolo
MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa Salim Asas ameichangia jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi ( UWT) wilaya ya Kilolo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano ya hadhara.
Asas ametoa ahadi hiyo Leo wakati akifungua kikao cha baraza kuu la UWT Wilaya ya kilolo. Alisema kuwa lengo la kusaidia jumuiya hiyo ni kuitaka ijitegemee pia kuwa na miradi yake.
Kwani alisema ameona ni vema kuiwezesha jumuiya hiyo kupata ndoano kuliko kuipa samaki na kuwa kwa kipindi chake chote cha miaka mitano atakayokuwepo madarakani ataichangia jumuiya hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi huo
"Ahadi yangu nitapaswa kuiweka katika maandishi ili familia yangu ijue pale nitakapo tangulia mbele za Haki ahadi hii iweze kutekelezwa na familia maana hatujui la kesho"
Hata hivyo alipongeza jitihada za UWT wilaya ya Kilolo kwa kuwa na mipango ya kimaendeleo kwa jamii tofauti na vyama vya upinzani ambavyo mipango yao ni maandamano na vurugu.
Usikose kusoma gazeti la RAI undani wa habari hii au tembelea Chanel yetu ya YouTube: matukiodaima 

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa,ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa wa Iiringa Salim Asas akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo, kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT wilayani humo.




Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga ( NEC)Salim Asas akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 5 mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT
Asas akipongezwa kwa mchango wake 

No comments: