NA MWANAHAMISI MSANGI, WMVU
WIZARA
ya Mifugo na Uvuvi imeunda timu ya wataalamu 15 iliyopo katika mikoa 26
ya Tanzania bara ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Dk.
Maria Mashingo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa zoezi la upigaji
chapa mifugo yote nchini kabla ya kufika tarehe ya mwisho ya muda wa
nyongeza wa Januari 31 mwaka huu.
Timu
hiyo ya wataalamu imeanza kutekeleza majukumu yake Januari 4 mwaka huu
ambapo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Maria Mashingo
wilaya 30 ambazo bado hazijaanza zoezi la chapa na zimetiliwa mkazo
katika ufuatiliaji ikiwemo Monduli, Kilwa, Liwale, Ruangwa, Mafia.
Aidha,
Wilaya nyingine ni Sikonge, Tabora, Urambo, Mwanza, Ilemela Manispaa,
Magu, Ukerewe, Buchosa, Tarime, Kyerwa, Ngara, Newala, Newala Mjini,
Tandahimba, Nanyamba, Mtwara, Mikindani Manispaa, Masasi, Masasi Mjini,
Nanyumbu, Moshi DC, Hai, Same, Rombo, na Kigamboni.
Dk.
Mashingo amesema suala la upigaji chapa mifugo lipo kwa mujibu wa
Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo Namba 12 ya Mwaka
2010 ili kudhibiti magonjwa ya mifugo pamoja na wizi wa mifugo,
kuimarisha usalama wa afya na mazao ya mifugo pamoja na kudhibiti
usafirishaji na uhamaji holela wa mifugo.
Amesema
jumla ya ng’ombe millioni 19, 219,487 sawa na theluthi mbili ya ng’ombe
wote milioni 28, 829,231 walioko nchini ambapo mpaka sasa jumla ya
ng’ombe milioni 7, 701,661 sawa na asilimia 38.5 ndio wamepigwa chapa
ambapo wamechangia kiasi cha shs. Bilioni 3, 700,830,500 kwa malipo ya
Tsh 500 kwa kila ng’ombe.
Hivyo,
Tathmini iliyofanyika kutokana na taarifa zilizokusanywa kutoka
halmashauri zinaonesha kwamba, kati ya malengo waliojiwekea, Halmashauri
62 wamepiga chapa zaidi ya asilimia 50; Halmashauri 43 zimepiga kati ya
asilimia 10 hadi 50; Halmashauri 23 zimepiga chini ya asilimia 10 na
Halmashauri 30 hazijaanza lakini ziko kwenye maandalizi.
Ametaja
baadhi ya changamoto zilizochangia kuathiri utekelezaji wa zoezi la
chapa ni wafugaji kukataliwa kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa
ni wavamizi na wahamiaji haramu katika Wilaya za Kibiti, Rufiji,
Sumbawanga, Tanganyika, Kibondo.
Pia
kutofautiana kwa gharama za uchangiaji ambapo baadhi ya wafugaji
waliogomea kiwango cha sh 1000/= ambacho ni kinyume na kiwango elekezi
cha sh 500/= kwa kila ng’ombe mfano katika Wilaya za Chunya na
Tanganyika. Vilevile
fedha zilizochangwa kugharamia zoezi la chapa kutotolewa kwa wakati
katika baadhi ya Halmshauri ikiwemo Mbarali na Misungwi hivyo kukwamisha
utekelezaji wa kazi hiyo.
Timu
hiyo ya watalaamu imegawanyika katika makundi saba kwenye mikoa ya
Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Pwani,
Dar es Salaam.
Mikoa
mingine ni Tabora, Katavi,Rukwa, Kigoma, Shinyanga, Simiyu,
Mara,Mwanza, Geita, Kagera, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi
na Mtwara.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa
ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 ya Wizara hiyo walioko katika
mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatilia na kusimamia kikamilifu zoezi la
upigaji chapa ambapo Dk Mashingo alisema mifugo itakayokuwa haijapigwa
chapa hadi kufikia Januari 31 mwaka huu haijulikani Serikali nini kuhusu
mifugo hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha
wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili
kuepuka kuharibu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika
Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya
timu ya wataalamu 15 iliyoundwa na Wizara hiyo kufuatiliaji na kusimamia
upigaji chapa kabla ya Januari 30 mwaka huu
No comments:
Post a Comment